LESENI ZA ZAMANI MWISHO MARCH 31
Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohammed Mpinga amewataka
madereva wote nchini kubadilisha leseni zao za zamani kwa kuwa zimebaki
siku saba tu zoezi hilo kumalizika, vinginevyo hatua za kisheria
zitachukuliwa.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mpinga alisema Machi 31, mwaka huu itakuwa mwisho wa madereva wote kutumia leseni za zamani, na kwamba kwa waliokuwa bado hawajabadilisha wafanye hima kubadilisha ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza.
“Machi 31 ndiyo mwisho na hatutaongeza muda wa kubadilisha leseni, hivyo wananchi wakae wakijua, nawaomba watumie wiki hii moja iliyobaki kubadilisha leseni zao,” alisema Mpinga.
Alisema ifikapo Aprili Mosi mwaka huu wanataka kuona kila dereva anakuwa na leseni mpya, kwani za zamani hazitatambulika na kwamba atakayebainika na leseni ya zamani atachukuliwa hatua za kisheria.