Wataalamu wa teknolojia waichambua video ya Lwakatare, baadhi wadai ni halisi!
WAKATI
umma wa Watanzania ukiwa na kiu ya kutaka kufahamu ukweli kuhusu video
inayomuonyesha Mkuu wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) akipanga kufanya vitendo vya kigaidi, ikiwa ni pamoja na
kudhuru watu mbalimbali, wakiwemo waandishi wa habari, wataalamu wa
masuala ya Teknolojia ya Mawasiliano, wakiwemo wale wa kutoka katika
taasisi mbalimbali zinazoheshimika nchini, wameichambua video hiyo.
Miongoni mwa wataalamu hao ni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dar es Salaam Information Technology (DIT), pamoja na wataalamu wengine, wakiwemo watayarishaji na waongozaji waliobobea katika masuala ya filamu nchini.
Gazeti hili lilifanya mahojiano na wataalamu hao ambao wamechambua uhalisia na kile kilichomo ndani ya video hiyo, ikiwa ni pamoja na maneno anayosikika akizungumza Lwakatare kwa kuzingatia uzoefu wao katika masuala ya teknolojia.
Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Wakichambua video hiyo, wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutoka kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano (IT), waliichambua video hiyo kwa kulinganisha uchanganyaji wa picha na maneno katika video nyingi zinazoonekana katika televisheni nyingi, hasa tamthilia za Kifilipino.
Wataalamu hao, wakiwemo wachanganya picha, wakifafanua kuhusu hilo, walisema kukua kwa teknolojia duniani hakuna kinachoshindikana katika kuchanganya picha bandia na ikaonekana kuwa halisi.
Kwamba licha ya vyuo vingi ya hapa nchini kutokuwa na uwezo wa kutoa taaluma hiyo kwa hali ya juu, lakini wapo Watanzania waliopata mafunzo hayo kutoka vyuo vikubwa vilivyoko nje ya nchi, hivyo lolote linaweza kufanywa kwenye teknolojia ya mawasiliano hapa nchini.
Katika kuchambua video hiyo ya Lwakatare, mmoja wa wataalamu hao aliyejitambulisha kwa jina la Athumani Hamis, alisema mazingira yanayoonekana katika video hiyo ni halisi.
Alisema wakati video hiyo inarekodiwa, kuna uwezekano watu hao walikuwa katika maongezi ya kawaida, kumbe mmoja kati yao alikuwa na kamera na kuchukua picha ambapo baadaye alikuja kuunganisha na sauti na kuonekana kuwa ni kitu halisi kilichofanyika.
Hamis alisema licha ya mazingira kuonekana kuwa ni halisi, lakini pia kuna uwezekano wa teknolojia kutumika katika uchanganyaji wa sauti na picha na mtazamaji akaona kuwa ni kitu halisi.
Hivyo kuhusu sauti inayosikika Lwakatare katika video hiyo, alisema hawezi kusema ni halisi au si halisi, kwa sababu pia ipo njia ya kuitengeneza jinsi mtu anavyotaka.
Chuo cha Dar es Salaam Information Technology (DIT)
Jopo la wataalamu kutoka chuo hicho kwa upande wao walisema sauti anayosikika Lwakatare katika video hiyo ni halisi, kwa sababu mdomo na maneno anayotamka vinaendana.
Kuhusu mazingira yanayoonekana katika video hiyo, wataalamu hao wanasema ni halisi na hayajahaririwa kutokana na kusikika kelele nyingine wakati video hiyo ikichukuliwa.
Mmoja wa wataalamu hao wa DIT, Mariam Jaha, akifafanua kuhusu sauti inayosikika katika video hiyo, alisema kama sauti hiyo isingekuwa halisi kwa maana ya ‘kupikwa’ studio, kelele nyingine zinazosikika katika video hiyo zisingesikika.
“Katika kurekodi picha kwanza na baadaye kuingiza sauti ukiwa studio lazima kelele zifutwe, ili kitu kiwe na ubora lakini kwa video hiyo kelele ziko wazi, hili ni pamoja na picha kuonyesha juu ya paa na chini kutokana na kamera kuhama wakati wa kurekodi,” alisema Jaha.
Mtaalamu mwingine ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini, ambaye hoja zake nyingi anakubaliana na Jaha alisema video hiyo ni halisi kutokana na kila kitu kuonekana katika mpangilio na kwamba hata mhusika (Lwakatare) anaonekana alikuwa anajua kuwa anarekodiwa, ndiyo maana wakati mwingine alikuwa akionekana akikwepa kuiangalia kamera mara kwa mara.
Mbali na hilo, anasema hata kamera iliyotumika kurekodi tukio hilo ilikuwa na uwezo mkubwa, kutokana na kumchukua vyema (Lwakatare) kwa kumjaza na hata picha kuonekana katika hali ya ubora.
Uchambuzi wa mtayarishaji na muongoza filamu
Mmoja wa watayarishaji na muongozaji wa filamu wa miaka mingi nchini, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, kwa upande wake naye alisema mazingira ambayo video hiyo ilirekodiwa ni halisi na wala si ya kutengeneza.
Alisema kwa miaka yote aliyofanya kazi hiyo hakuna ‘feki’ inayokuwa katika uhalisia kama unaoonekana katika video hiyo pasipo mtazamaji kugundua.
Mtaalamu huyo anachambua zaidi akisema video inavionyesha viungo vya muhusika (Lwakatare) vikiwa na ushirikiano wa karibu kwa maana ya macho na maneno yanayotamkwa pamoja na vitendo vya mikono.
Akichambua zaidi, alisema wakati video hiyo inarekodiwa, inaonyesha kulikuwa na watu zaidi ya wawili, akiwemo mchukua kamera, ambaye alimwelezea kuonekana kuwa ni mtaalamu zaidi.
Pia katika kuiangalia video hiyo, alisema amegundua kulikuwa na mawasiliano baina ya subject (mhusika) na mtu wa kamera, ingawa kuna uwezekano kuwa aliichukua video hiyo akiwa kaificha katika kitambaa chepesi cha mkononi na kuibana vyema katika mkao ambao alikuwa amekaa pasipo mhusika kushituka.
Alisema weusi unaoonekana katika video hiyo inadhihirisha kwamba si bandia na umetokana na mchukuaji kuiweka kamera ili iweze kuchukua upana mkubwa ‘wide screen’, kwamba hii inamaanisha mchukuaji picha ni mtaalamu.
Mtayarishaji huyo wa filamu nchini akichambua zaidi, anasema mchukuaji wa video hiyo alitumia taa ya kawaida, ingawa kitaalamu katika kuchukua picha inatakiwa kutumia taa za video.
Alisema kitaalamu haiwezekani kubadili mwanga halisi unaoonekana kwenye picha ya video, na hii inadhihirisha kivuli cha mhusika kinachoonekana katika video hiyo, hali kadhalika vitu vinavyoonekana kwa nyuma ‘back ground’.
Mtaalamu huyo anasema ikitokea kama video hiyo ni ya kutengeneza, basi mwanga na ‘back ground’ huwa haviendani.
Hata hivyo, gwiji huyo wa kutengeneza filamu nchini anasema kamera iliyotumika kuchukua video hiyo ni ya kawaida, kama vile simu au kamera ndogo na kwamba si kamera za kawaida za kuandalia filamu ambazo huwa zinawekwa katika stendi yake.
Anasema kamera hiyo haikuwekwa kwenye stendi, ndio maana mchukuaji picha wakati fulani anaonekana kutikisika na kuonyesha juu ya paa la nyumba, hali inayoonyesha uhalisia ulikuwepo.
Mtaalamu huyo anakwenda mbali zaidi na kusema mchukua video huyo hakuwa katika mstari sawa ‘horizontal line’ bali alitumia pembe ya chini kidogo kutokana na muonekano wa video hiyo kwamba aliyekuwa akirekodiwa hakuwa na taarifa, na kwamba mchukuaji ana utaalamu wa hali ya juu wa kucheza na kamera.
Mtaalamu kutoka chuo kingine
Mtaalamu wa teknolojia kutoka katika chuo kimoja ambacho hakutaka kitajwe gazetini, alisema kuwa kuna uwezekano wa kuingizwa uongo mwingi katika sinema mbalimbali, lakini kwa hapa nchini, utaalamu huo haujafikiwa kwa kiwango kikubwa.
Alisema ukitaka kumtengeneza mtu ‘feki’ aonekane kwenye video kwa sura yake halisi, ni gharama kubwa kwa sababu hata kama ikipatikana picha ya mtu huyo akiwa katika kikao na mtu mwingine wakati wa kuingiza sauti inapaswa kuhakikisha midomo inakwenda sambamba na maneno na kazi hiyo ili kuifanya ikamilike vizuri inarekebishwa kwa kutumia ‘software’ zinazopatikana kwa kiwango cha kati.
Mbali na hilo, pia alisema kuna utaalamu wa kumbadilisha mtu kwa kumfanyia ‘Plastic Surgery’ ili aonekana kama yule unayemkusudia, lakini ni gharama kubwa, na hapa nchini hawawezi kumudu, lakini pia Tanzania haijafikiwa na utaalamu wa hali ya juu kama huo.
Hivi karibuni, Lwakatare pamoja na Ludovick Joseph Rwezaura walikamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Machi 18 mwaka huu na kusomewa mashitaka manne, likiwamo la ugaidi na kula njama ya kutenda kosa la jinai la kutoa sumu kwa nia ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi, Dennis Msacky.
Hati ya mashitaka iliyosomwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Prudence Rweyongeza, mbele ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru, ilieleza kuwa washitakiwa hao walifanya kosa la kula njama na kutenda makosa ya jinai kunyume na kifungu cha 384 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16, iliyofanyiwa marekebisho 2002.
Hata hivyo, washitakiwa waliachiwa huru Machi 20 mwaka huu na kukamatwa tena ndani ya viunga vya Mahakama hiyo na kusomewa mashitaka yaleyale na wakili Rweyongeza, mbele ya Hakimu mwingine, Aloyce Katemana.
Gazeti la Mtanzania Jumapili.