Bukobawadau

ALICHO KISEMA MBUNGE WA NZEGA MH.HAMISI KIGWANGALLA (CCM)

Ni jambo la kawaida kwa mtu kutamani kuwa Rais wa nchi yetu. Lakini je unaguswa na matatizo ya wananchi? Unaguswa na kadhia wanayopata akinamama wajawazito kule labour ward wanapolazwa kwenye kitanda kimoja wawili wawili? Unaguswa na na adha wanazopata watoto wa shule kukosa vitabu, madawati, walimu na kusoma na njaa mpaka jioni? Unaguswa na kero za walimu na madaktari? Unaguswa na adha ya wananchi wanaoamka hawajui leo watapata wapi riziki ya kulisha matumbo yao na familia zao? Unaguswa na haya na ambayo sikuyataja hapa? Haitoshi tu kwa wewe kuguswa na mambo haya, je una uelewa wa kutosha wa namna ya kuleta ufumbuzi wa changamoto hizi? Haitoshi tu pia kuwa na uelewa, lakini je una utashi na utayari wa kuleta ufumbuzi wa kadhia hizi kwa haraka? Ni haki kutamani kuwa Rais lakini tuwe na majawabu ya maswali haya magumu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau