Bukobawadau

HARUSI YA HOME BOY YAFUNIKA ILE MBAYAA,NI KIJANA WA 'ABAJALIZI' MOHAMED KASSIM NA BI BI RAYAH KORONA MUSSA

Hivi ndivyo wadau walivyo towa support ya nguvu kwa kijana wa Nyumbani , Ni Mtoto wa Mzee Kassim maarufu kama 'MOHA ABAJULIZI' ukipenda  Ustaadh Mohamed Kassim.
Baada ya shughuli ya ndoa iliyofanyika nyumbani kwao Bibi Harusi,shughuli iliendelea  Nyumbani kwa Mzee Kassim  baba mzazi wa Bwana Harusi maeneo ya Kibeta ndani ya Manispaa ya Mji wa Bukoba.
Ni shughuli iliyochukua kasi imekuwaa top story katika vyombo mbalimbali vya habari, Radio station kadhaa Tv zinazopatikana katika ukanda huu, Blogs na 'OLUGAMBO' kibao kitaani.
 Ni shughuli iliyowashirikisha wadau mbalimbali wa lika tofauti

Wageni wakiwasiri eneo la tukio.
Bw.Harusi Mdau Mohamed Kassim.
Mzee Kassim,Baba Mzazi wa Bw. Harusi

Ustaadh Mwalimu Adinin akitekeleza zoezi zima la kuwafungisha nikai maharusi wetu

Tayari imeandikwa kwa wana ndoa kuwa BUSU ni Sunna.
Familia ya Mzee Kassim katika picha ya pamoja , yaani Bw Harusi Mdau Moha na Dada zake

Action time

Picha maalum iliyochukuliwa kwa ajili ya kumbukumbu kwa faida yako wewe mdau msomaji na kwa faida ya kizazi kijacho,


Wasiliana na Bukobawadau kupitia 0715 505043,0754 505043au 0784 505045 viber pia tunapatikana BBM kwa pin  26F2A367 NA 234E5 DD7 au 0713 397241 Email bukobawadau@ gmail.com kwetu sisi kazi ndio msingi,kuwa karibu na wadau ni utamadun,Uzalendo umesimama kama sera!!!
Maharusi wetu wakiwa wamejipanga vyema  ni 5,4, 2 mfumo mpya wa Jose Mourinho

USIKU SHUGHULI ILIWEZA KUENDELEA NDANI YA UKUMBI BABU KUBWA UKUMBI WA KISASA WA LINAS NIGHT CLUB .
Shangwe ndelemo, vikeleshendo, mapana yenye swagar za whatsApp ilikuwa mle mle ndani ya Kisima cha burudani,ndani ya Kigata cha KISASA Linas Night Club.
Mdau Zakia Mwaza Kassim, mdogo wa Bw Harusi pichani akiwa katika pozi lenye kila dhamila
Wazazi wa Bwana Harusi pichani Mr & Mrs Kassim
Kamati ya harusi hii ilisimama namna hii ikiwakirisha  'Nyeusi'Camera yetu imefanya yake na KUAKIKISHA kila mwananzengo alipatia  sana katika Kiatu sehemu muhimu inayo washinda wengi.(makofi kwao kimoyomoyo mdau)
Mwanzo wa masham sham ndani ya Linas Club, wakiingia wapambe wa maharusi wetu.
Hakika Shughuli ni watu, pichani  anaonekana Mdau Mbishi Jerry akifanya yake katika kuwapa shavu maharusi wakiwa wanaingia ukumbini.
Maharusi wetu wakikata utepe.

Sehemu ya wadau ukumbini.

Kila mgeni aliweza kupata kile kinachostahili.
Bila shaka mara kwa mara umekua ukifutilia na kuona umoja wa Bukoba Veteran,moja ya faida katikaumoja huo ndiyo kama hivi,wapo pamoja kwa shida na raha.
Zawadi kutoka Bukoba Veteran.
 Kitendo kinacho endelea ni kukabidhi zawadi
Ingawa utaratibu wa zawadi kwa maharusi imezoeleka , ila kuna mikato, swaga,utofauti mkubwa wa kiubunifu katika matukio yanayokuwa yakiendelea Mjini bukoba, Hii itachukuliwa tu na wani ni bonge la bakoola!!

Mdau Mveteran Evody aka Chinga Boy akitoa neno.
Ndugu wa Bwana Harusi wakitoa zawadi zao.


Ikafika wasaa wa kamati ya maandalizi ya harusi kukabidhi zawadi yao
Kamati makini ikikabidhi zawadi
 Kamati ikipambwa na bonge la show kutoka na mshereheshaji wa shughuli hii, Mc Magoma kutoka jijini Mwanza.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa maharusi wetu.
Kutoka THT msanii Amini Mzee wa 'Omtima Wange ni Wewe'akifanya yake.
Muonekano wa zawadi.
 Ofisi anayo fanya kazi Chini ya Mkurugenzi Rukia nayo iliweza kupata fulsa ya kutoa zawadi yake.
Msemaji wa Kampuni husika.
 Da' Mai na maharusi wakionyesha kufurahishwa na maeno matamu kutoka kwa msemaji wa Kampuni.


Mambo ya burudani...!!

  Ni mara chache sana bk hii kupata time ya kusakata

Wakisakata lumba Mwenyekiti wa Kamati ya harusi hii Ndg Jamal Kalumuna(JK) na Mkewe Bi Jamila.
Hakiwa mambo ni bam bam kama unavyoweza kujionea.
Pichani ni Da' Lilian Peter Mwise na Bi Salome Mama Baraka( Chui na London) guu guu.
kila pahala na watu wake na sie tunaamini katika hilo.
 'Ni wewe unaye nifanya nilie, ni wewe unayenifanya nipaga' hayo si maneno yangu mimi bali ni mistari kutoka kwa msanii AMIN aliye kwenye chat ya juu katika tasnia ya uimbaji.
 Mdau Jane Zachwa katika picha ya kumbukumbu na Bi Harusi wetu Bi Rahah Mussa.
Mzee Kassim Baba Mzazi wa Bw. Harusi akitoa neno.
 Kuelekea mwisho ,Unaweza kupata habari zetu kiujumla kupitia twiter @bukobawadau, na video zetu kupitia account yetu ya you tube.vilevile unaweza kujiunga kwenye facebook page yetu.
BUKOBAWADAU BLOG Tunawapongeza maharusi hawa kwa uamuzi wao!!.
 Mdau Mama Matungwa Mkurugenze The Walkgard  Hotel akichukua picha ya kumbukumbu 
Mkurugenzi wa Linas Night Club, Mdau Mtensa.
 Pitia Older Post kupata matukio ya muda mchache uliopita.

Wasiliana na Bukobawadau kupitia 0715 505043,0754 505043au 0784 505045 viber pia tunapatikana BBM kwa pin  26F2A367 NA 234E5 DD7 au 0713 397241 Email bukobawadau@ gmail.com kwetu sisi kazi ndio msingi,kuwa karibu na wadau ni utamadun,Uzalendo umesimama kama sera!!!

Next Post Previous Post
Bukobawadau