MKASA WA KUOTA NDEVU KWA MWANAMAMA MARIAM
Mariam,mwanamke
aliyezaliwa nchini Ujerumani amepatwa na mkasa wa kuota ndevu nyingi
kama mwanaume.Awali alikuwa akiziondoa ndevu hizo kwa njia mbalimbali
lakini ilipofika mwaka 2008 aliamua kuachana na vifaa vyote vya
kuondolea ndevu na kuacha ndevu hizo zikue ambapo kwa madai yake,baada
ya kuziachia ndevu hizo anajisikia kujiamini zaidi kuliko kipindi
alichokuwa akiziondoa.Tatizo hilo la kuota ndevu mithili ya mwanaume
alilipata miaka 28 iliyopita mara tu baada ya kujifugua mtoto wake wa
kwanza.Majaribio mbalimbali ya kimaabara yamefanyika ili kuona ni sababu
zipi zinazomfanya mwanamke huyo kuota ndevu nyingi kiasi hicho lakini
mapaka sasa hakuna kilichogundulika.