CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA KAGERA (KPC)KATIKA MKUTANO MKUU
Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kagera(KPC)
kimefanya Mkutano Mkuu wa mwaka,ambapo pamoja na mambo mengine kimejadili na
kupitisha wanachama wapya.
Katika Mkutano huo uliofanyika ukumbi wa St Francis,mjini Bukoba pia wanachama walijadili taarifa mbali mbali zilizowasilishwa na uongozi na kufikia maazimio mbalimbali.
Miongoni mwa maazimio ya Mkutano huo,ni kuendeleleza
umoja kwa ajili ya ustawi wa chama,huku waandishi wa habari wakikumbushwa
kufanya kazi zao kwa maadili na weredi.
Pia Mkutano huo ulimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera
Kanali Mstaafu Fabian Massawe,pamoja na wadau wengine wa Kagera Press Club
ambao kwa nyakati tofauti wameunga mkono juhudi za Umoja huo ili kufikia
malengo yake.
Baadhi ya waandishi wa habari katika matukio
mbalimbali ndani na nje ya ukumbi,Baadhi wakikagua vifaa vya kisasa vya kazi na
wengine wakitoa michango yao.
Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa Ndg Phinias Bashaya na Mwenyekiti John Rwekanika
Method Kalikila wa Gazeti la Rumuli na Livinus Feruzi wa Gazeti la Majira wakifuatilia mjadala
Ayoub Mpanja(Radio Free Africa)Ashura Jumapili-Tanzania Daima
Mathias Byabato-Channel Ten
Antidius Kalunde-Tanzania Daima
Ashura Jumapili-Tanzania Daima
Winrida Saimon Mwandishi wa Gazeti la Ijawebonele linalomilikiwa na ELCT/Dayosisi ya Kaskazini Magharibi
Meddy Mulisa-Mhariri Radio Kasbante na mwandishi wa Daily News akinukuu mambo muhimu wakati wa mkutano.
Anaonekana Jonas Mchunguzi-Mwandishi na mtaalamu wa kupiga picha za habari na matukio akikagua kamera ya kisasa.
Prudence Kibuka-Nipashe akiendeleza majadiliano na wenzake wakati wa mapumziko.
Picha kwa Hisani ya Phinias Bashaya