Bukobawadau

TASWIRA;MATUKIO YA KUAPISHWA KWA RAIS WA AWAMU YA NNE NCHINI KENYA,RAIS UHURU KENYATTA

Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akiapa mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake.
Hii ni baada ya Uhuru kumshinda Raila Odinga katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe nne mwezi Machi
Wageni mashuhuri wakiweno marais wa nchi kadhaa za Afrika pamoja na wanadiplomasia na maelfu ya wananchi walishuhudia sherehe hizo katika uwanja wa michezo wa Kasarani viungani mwa mji wa Nairobi.
 Rais wa Kenya Uhuru Kenyata na first lady Margaret Kenyatta
 Rais Uhuru Kenyatta na first lady Margaret Kenyatta
 Uhuru Kenyatta akijiandaa kula kiapo chake
 Rais mpya wa awamu ya nne nchini Kenya,Mh Uhuru Kenyatta akisoma hotuba yake mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake
 William Ruto makamu wa Rais wa Kenya akisaini
Aidha Kenyatta ndiye rais mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuongoza nchi. Ana umri wa miaka 51 na ni mwanawe rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta.

 Rais Uhuru Kenyatta akikabidhiwa upanga na nakala ya katiba ya Kenya na rais mstaafu Mwai Kibaki ishara kuwa amekuwa amiri mkuu wa majeshi ya Kenya.
 Jaji Mkuu wa Kenya Willie Mutunga amtambulisha rais mteule wa Kenya kwa wakenya kuambatana na sheria na matakwa ya katiba ya Kenya na kuchukua kiapo cha kushuhudia kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta










Wakimpungia mikono


Rais Mwai Kibaki anayeondoka madarakani anakagua gwaride la heshima

Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete pichani kulia, akisalimiana na Rais Mpya wa Kenya Rais Uhuru Kenyatta
 Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto na Mkewe pembeni wakifutilia moja ya tukio.
 Habari hii imedhaminiwa na Windhoek Lager
 First Lady wa Kenya  Margaret Kenyatta na First Lady wa Tanzania Mama Salima Kikwete.
 ais mstaafu wa awamu ya tatu nchini Kenya Bwana Mwai Kibaki akisalimiana na Rais wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete



 Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye sherehe ya kuapishwa Rais wa awamu ya nne nchini Kenya iliyofanyika kwenye uwanja wa Kasarani,jijini Nairobi Sherehe hizo zimehudhuriwa na Marais kutoka nchi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh Jakaya Mrisho Kikwete,Mabalozi na watu wengine mbalimbali.
 Rais Uhuru Kenyatta akiwapungia maelfu ya watu waliofika kushuhudia kuapishwa kwake.
Raila Odinga hakuhudhuria sherehe hizo baada ya jitihada zake kutaka mahakama ya juu zaidi kubatilisha matokeo ya uchaguzi kukosa kufua dafu.




Next Post Previous Post
Bukobawadau