Bukobawadau

HALI YA MAJI KAGERA SIO YA KURIDHISHA

HALI ya upatikanaji wa huduma ya maji mkoani Kagera sio ya kuridhisha kufuatia asilimia kubwa ya vituo vya kutolea maji kuharibika na hivyo kupelekea wananchi kukosa huduma za maji. 
Akiwasilisha taarifa ya uhakiki wa huduma ya maji kwa upande wa mkoa wa Kagera kwa wadau wa maji, Meneja mradi wa maji na nishati wa shirika la KADETFU Augustine Angelo alisema uhakiki huo umebaini kuwa zaidi ya nusu ya vituo vilivyojengwa kutolea maji vimeharibika na hivyo kufanya baadhi ya watu kukosa huduma ya maji.
 
Uhakiki wa huduma ya maji mkoa wa Kagera umeendeshwa na shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia sekta ya maji, mazingira, kilimo, ufugaji, nishati na afya katika mkoa wa Kagera (KADETFU) kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la uholanzi (SNV).
 
Katika uhakiki huo umebainika kuwa licha ya wafadhili na wadau mbalimbali wa maendeleo kutumia fedha nyingi katika uwekezaji wa miradi ya maji,bado miradi hiyo imekuwa ikiharibiwa na kuhujumiwa na baadhi ya watu.
Next Post Previous Post
Bukobawadau