Bukobawadau

MCHEZO WA JANA KATI YA SIMBA, YANGA WAINGIZA MIL 500/=

Pambalo la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom
lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh.
500,390,000.

Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo
msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa
viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na
sh. 30,000.

Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.

Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo
waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati
kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh.
123,515,000.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81,
tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi
sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
14,708,415.12.
Next Post Previous Post
Bukobawadau