Bukobawadau

MELI MAALUMU KUTUMIKA KUTOA MATIBABU KATIKA VISIWA VYA WILAYA YA MULEBA

 Mkuu wa Wilaya ya Muleba Rembres Kipuyo akifungua Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Wilaya ya Muleba.
 Diwani wa Kata ya Buganguzi Onesmo Niyegila akihoji halmashauri kushindwa kutengeneza daraja linaloiunganisha Kata yake na Hospital teule ya Rubya.
 Diwani wa Kata ya Muhutwe Justus Magongo akiwasilisha taarifa ya kata yake tayari kwa majadiliano.


Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani  Kagera limeidhinisha mpango wa kutoa huduma za matibabu kwa kutumia meli maalumu kwa wananchi wanaoishi katika mwambao wa visiwa vinavyozunguka Wilaya hiyo.

Madiwani hao wamesema  kuwa wananchi wengi wanaoishi katika visiwa vinavyozunguka wilaya hiyo ndani ya Ziwa Victoria wanakabiliwa na adha  ya kukosa huduma za matibabu na mpango wa kutumia meli maalumu utaokoa maisha ya wananchi walioko katika visiwa hivyo.

Kambi ya upinzani katika Baraza hilo kupitia kwa msemaji wake ambaye ni Diwani wa Kata ya Kishanda  Alfred Pastory  amesema kambi hiyo inaunga mkono mpango huo kwani utaokoa maisha ya wananchi ambao hupoteza maisha kwa kukosa huduma za matibabu.

Awali akifungua Mkutano wa Baraza hilo Mkuu wa Wilaya ya Muleba Rembres Kipuyo amewataka madiwani  kuwaeleza wananchi katika maeneo yao jinsi Serikali inavyojitahidi kutatua  kero zao kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Pia amesema kuwa pamoja na Serikali kutoa mamilioni ya fedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali,wananchi wengi katika ngazi za vijiji na Kata hawana taarifa za kutosha juu ya miradi inayotekelezwa katika maeneo yao.
Muonekano wa stendi ya Mabasi Muleba.
 Hii ni hali ya usafiri kati ya Muleba na Bukoba

Wanadada katika pitapita zao , maeneo ya Muleba.
Next Post Previous Post
Bukobawadau