Bukobawadau

MKUU WA MKOA WA KAGERA KANALI FABIAN MASSAWE ATOA MIEZI 6 KWA VIONGOZI WA SERIKALI NA VYAMA VYA SIASA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUJENGA NYUMBA BORA ZA KUISHI

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabiani Masawe akiangalia moja ya nyumba siyobora wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo wilayani Biharamulo ,mkoani Kagera
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabiani Masawe amewataka Viongozi wa Wilaya Mkoani Humo ,ndani ya miezi sita kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo hasa ardhi na misitu kujenga nyumba bora za kuishi kuliko zile za matembe kuonekana kuwa maskini bila kufanya kazi na kujiletea maendeleo. “Makazi hayo yajengwe kwa kutumia matofali yasiyochomwa na kuezekwa kwa miti na nyasi kisha waongeze uzalishaji wa mazao ya kilimo na ufugaji ndani ya mwaka mmoja waezeke kwa mabati” Alisema Masawe. Akiwa katika ziara ya kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika wilaya za Biharamulo na Ngara mkoani Kagera.

Kanali Masawe alishauri ukusanyaji wa michango ya wananchi katika kujiletea maendeleo mkoani Kagera , uzingatie kutolewa rasilimali zinazopatikana katika mazingira yao kuliko madai ya fedha ambazo huliwa na watendaji wasio waaminifu katika Vijiji na Kata kwa kukosa kuwapatia stakabadi halali wala taarifa ya mapato na matumizi. Aliwataka Maafisa ugani kuhakikisha wanafanya kazi zao Vijijini kuwasaidia utaalamu Wakulima na Wafugaji ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuwachukulia hatua Walevi saa za kazi pamoja na Wasiowajibika ipasavyo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau