Bukobawadau

MOJA YA HABARI ILIYOCHUKUA KASI KWENYE VYANZO MBALIMBALI LEO MEI 15,2013

Dk Slaa na Nape katika studio za ITV, Mikocheni.
Kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya kitaifa ambapo wasemaji wakuu wa mjadala huo walioalikwa walikuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya Siasa, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbroa Slaa.

Kwamba, kutokana na udhuru wa Ndg. Kinana kusafiri kuelekea Dodoma kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu jana na pia kubanwa na majukumu mengine muhimu ya Kichama na Kitaifa, alimuagiza Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM, ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo.

Kwamba, baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo Mikocheni asubuhi ya leo, Nape alipokutana na Dk Slaa alimweleza kuwa anamuwakilisha Katibu Mkuu wake katika mazungumzo hayo.

Kwamba, baada ya kusikia kauli hiyo, Dk Slaa alihamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa sababu anamtaja vibaya kwenye mikutano yake.

Kwamba, jutihada za kumsihi aaendelee na mazungumzo hayo muhimu na kipindi hicho kwa Watanzania, Dk Slaa aligoma na kuondoka.

Kwamba, waliodadisiwa kuhusiana na tukio hilo, walisema Dk Slaa atakuwa amemwogopa Nape katika mjadala/mazungumzo hayo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau