Bukobawadau

HABARI MBALIMBALI KWA MKUTASARI

"Kinacholiponza taifa letu hivi sasa, ni viongozi wenye kupenda kuropoka na kusema sema badala ya KUZUNGUMZA. Hawajisumbui kufikiri kwa kina hoja mbele yao, maana wanaamini wanajua kila kitu. Hawapendi kusumbua akili zao walau kufanya marejeo ya matendo, maneno au maamuzi yao yaliyotangulia, majibu yao yanategemea zaidi mood zao kwa muda huo na sio uzito wa kile wanachotakiwa kukijibia"
 - Counselor Rama Msangi
KAULI YA MH.PINDA BUNGENI LEO
Ukifanya Fujo umeambiwa usifanye hiki , ukaamua we kukaidi utapigwa tuu, mana hakuna namna nyengine mana lazima wote tukubaliane kuwa Nchi hii tunaiendeshwa kwa misingi ya Kisheria .. Sasa kama wewe umekaidi hutaki, unaona kama ni imara zaidi wewe ndio Jeuri zaidi , watakupiga tuu na mimi nasema muwapige tuu kwasababu hakuna namna Nyengine kwa kuwa Tumechoka sasa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Kuteuliwa, Joseph Mbatia, Bungeni Mjini Dodoma Juni 20,2013
Wabunge wa CUF wakimsindikiza Yussuf Salim Hussein (wapili kushoto) wakati alipoapa kuwa Mbunge, Bungeni Mjini Dodoma Juni 20,2013
 Mh. Pinda akiteta jambo na Mh Mbatia ndani ya ukumbi wa Bunge.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi kwenye viwanja vya Bunge MjiniDodoma Juni 20, 2013
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Freeman 
Mbowe na Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini,Godbless Lema wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa ilikuweza kutoa ushahidi wa tukio la bomu lililotokea kwenye mkutano wa kampeni wa chama hicho.Viongozi hao wanashikiliwa baada ya Mwenyekiti huyo kudai
anawajuwa waliolipua bomu na wanao mkanda wa tukio zima la ulipuaji huo wa Bomu kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani ulikuwa ufanyike Juni 16 jijini Arusha
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Benki ya kiarabau kwa maendeleo ya Afrika BADEA wakati wajumbe hao walipomtembelea na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.(picha na Freddy Maro)
Bajeti ya kodi.
Kuelekea katika shughuli ya Mazishi ya mwenyekiti wa BAWACHA kata ya Sokoni I Judith William Moshi, aliyefariki kwa mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha siku ya kufunga kampeni za chaguzi ndogo tarehe 15.06.2013, uchaguzi ambao ulikuwa ufanyike tarehe 16.06.2013.

Next Post Previous Post
Bukobawadau