Bukobawadau

HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA LWAKATARE KUPITIA FACEBOOK

Wasalaam waheshimiwa Wananchi,ndugu,jamaa na marafiki.Leo asubuhi,kesi yangu imeitwa katika mahakama ya mkazi Kisutu na kusikilizwa na Hakimu Mfawidhi Aloyce Katemana.Kesi imeahirishwa hadi 08/Julai/2013,ikiwa simu zangu bado ziko mikononi mwa polisi mpaka uchunguzi utakapokamilika.Pia,mshtakiwa wa pili Joseph Ludovick Rwezaula amerudishwa mahabusu mpaka atakapokamilisha nyaraka za dhamana ikiwa dhamana yake iko wazi.
Nichukue fursa hii kumshukuru kila mmoja anayeniombea na kunitakia kila lenye kheri.
Nawatakia siku njema Makamanda
Next Post Previous Post
Bukobawadau