Bukobawadau

KAMA UKUPATA KISA CHA HUYU MAMA ALIYEKAA JUU YA PAA KWA SIKU TANO KUZUIA NYUMBA YAKE KUUZWA NA BENKI YA TIB

 Huyu mama alikaa juu ya paa kwa siku tano tangu jumamosi kupinga nyumba yao kuchukuliwa na bank.Anasema mumewe alimdhamini mtu ambaye alichukua mkopo bank miaka mingi iliyopita na kushindwa kulipa mkopo huo.

Kwa mujibu wa maelezo yake , kesi yao bado ipo mahakamani kwani tayari yule mdaiwa kuna mali zake zilizotaifishwa.

Mdaiwa alikopa ml 240, wameuza nyumba zake 2 na mabasi mawili.Wadaiwa wanaomba kujua kiasi kilichobaki katika hilo deni ili watoe na kuuza nyumba yao.
 Gea alimfuata huko huko juu kumsikiliza...
Nyumba ipo mbezi Tangi bovu na inaeneo kubwa sana .Mama anasema hata akiuza si chini ya ml 500 iweje atolewe kwa ml 240 wakati mdaiwa nyumba zake mbili zimeshachukuliwa na mabasi mawili yale makubwa ya safari za mikoani yamechukuliwa .Hiyo ml 240 haijatimia tu?na kama bado kiasi gani kimebaki?
Ndani ya nyumba vitu walishachukua hao watu wa auction mart, ndani kweupe.Na wakati haya yakiendelea hakukuwa na amri yoyote iliyotoka mahakamani wala hawakuwa na kibali cha mahakama.
Chumba cha habari cha clouds fm kinafuatilia hapo bank ya Tanzania Investment bank(TIB) kujua chanzo cha tatizo maana wakati haya yakiendelea hiyo jana inasemekana hii nyumba ilikuwa imeshauzwa.

Jana hiyohiyo, mume wa huyu mama alikuwa mahakamani maana ilikuwa siku ya kesi kuendelea kusikilizwa. 

Taarifa zinadai kuwa Mumewe alirudi na oda maalum kutoka mahakamani kuwa nyumba hiyo isiguswe na vitu vyao virudishwe.

CREDIT;Dinamarios Blog
Next Post Previous Post
Bukobawadau