Bukobawadau

WATOTO WA SHULE ZA MSINGI MKOANI KAGERA WAONYESHA VIPAJI VYAO KATIKA MASHINDANO YA UMITASHUMITA




Katika kuhakikisha kuwa mkoa wa Kagera unarudi katika medani zake za zamani kwenye michezo, uongozi wa mkoa umeendelea na juhudi mbalimbali za kuendeleza na  kuibua vipaji vya watoto katika michezo mbalimbali  ili kuvikuza na kupata wanamichezo mahili hapo baadae.
Mkoa wa Kagera umezindua rasmi mashindano ya michezo  kwa shule  za  msingi (UMITASHUMITA) katika chuo cha Ualimu Katoke(Muleba) tarehe 05/06/2013 na kuhusisha Halmashauri za Wilaya zote  ambazo ni Muleba, Bukoba, Misenyi, Biharamulo, Karagwe , Kyerwa,  Ngara na Bukoba Manispaa.
Katika mashindano hayo jumla ya wanafunzi 754 wanashiriki michezo mbalimbali ikiwemo michezo ya mpira wa miguu, mpira wa mikono, mpira wa wavu, riadha, mpira wa netiboli,  miruko na mitupo.
Akizindua mashindano hayo rasmi Afisa Elimu Taaluma Bw. Renatus Bamporiki aliwasistiza wanamichezo waliofika kushindana na kuonyesha vipaji vyao, kushindana  kwa nidhamu kubwa na kuonyesha vipaji ili viweze kuendelezwa na kuuletea mkoa wa Kagera sifa kama ilivyokuwa zamani pia na kuwapatia ajira.
Kambi ya mashindano hayo itachukua siku nne kwa kila Wilaya kuonyeshana ujuzi na Wilaya zingine. Aidha kati ya wanamichezo 754 watachaguliwa wanamichezo 122 watakowakilisha mkoa katika ngazi ya kanda huko mkoani Kigoma kuanzia tarehe 13/06/2013.
Michezo hiyo inahusisha pia na wanafunzi wenye mahitaji maalum ambao wanatoka katika Manispaa ya Bukoba Mugeza Viziwi, pia kutoka Muleba katika shule za Kaigara na Rubya. Wanafunzi hao wenyenye mahitaji maalum wanasakata kumbumbu kwelikweli na kwa ufundi mkubwa sana.
Changamoto,  Vyama vya michezo huo ndiyo ulikuwa wakati mzuri wa kuona vipaji na kuweka mipango yakuviendeleza lakini hakuna hata kiongozo mmoja anayehudhuria mashindano hayo. Ili mkoa usonge mbale, viongozi wanahitaji kubadilika kimtazamo kwa  kuanza na watoto wadogo.
Ni matarajio ya mkoa kuwa watoto watakaochaguliwa katika mashindano hayo wataweza kuipeperusha bendera ya mkoa wa Kagera vizuri kuanzia ngazi ya mkoa, Kanda na Taifa.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013
Next Post Previous Post
Bukobawadau