Bukobawadau

KWA NGUGU ZETU WAHAYA LEO TUNAGUSIA MAANA YA NENO 'OKUBISILA'

Okubisila ni mila ya kujiandaa kwa mapokezi ya wageni mashuhuri, hata wale ambao hawakutaarifu mapema kuhusu ujio wao. Maandalizi hayo yanahusiana moja kwa moja na kahawa za kutafuna pamoja na pombe, kama ilivyoelezwa hapo juu, chini ya kipengele cha okutangilila.
Lakini katika mazingira ya magonjwa haribifu ya migomba (kama ‘mnyauko’) na kupungua sana miaka hii kwa zao kuu la ndizi kama chakula, Muhaya atabangaiza kuishi kwa kula mazao ya nafaka na mizizi (mihogo, viazi, magimbi, n.k- vyakula vya misimu (emyaka) visivyokuwa na hadhi kubwa kama ndizi, au vyakula vya kununua madukani (unga wa mahindi na mchele), ili mradi tu ahakikishe hakosi mikungu michache ya ndizi shambani mwake kwa ajili ya mgeni anayeweza kujitokeza wakati wowote.
‘Vyakula’ vinavyopatikana kwa msimu kama senene, huhifadhiwa maalum kwa ajili ya kukidhi mila hii. Na hakuna kitendo chochote cha heshima kubwa zaidi anachoweza kufanyiwa mgeni, kuliko kukarimiwa kwa senene. Labda tutoe mfano mmoja kuthibitisha thamani ya senene kwa Wahaya. Mwanamke ambaye mumewe amefungwa jela kwa miaka kadhaa, atafanya kosa linaloweza kuhatarisha ndoa yake asipochukuwa tahadhari ya kujiandaa kuwasilisha malimbikizo ya senene aliowahifadhi mnamo misimu iliyomkuta mumewe akiwa kifungoni!
Na kama tulivyoona awali, akifanya hivyo, atastahili ‘kulongolwa’ na huyo mumewe aliyerejea kutoka jela.
Next Post Previous Post
Bukobawadau