Bukobawadau

TASWIRA YA MKUTANO WA WILFRED MUGANYIZI LWAKATARE LEO VIWANJA VYA UHURU MJINI BUKOBA AFUNIKA

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Muganyizi Lwakatare akisalimiana na mmoja wa wafuasi wake waliojitokeza leo katika Mkutano wake wa adhala uliofanyika katika uwanja wa Uhuru mjini hapa.


Kikubwa alicho kisema Ndg Lwakatare ni kwamba amejifunza mengi kupitia jela hivyo ni muda sasa wa yeye kuitumikia familia yake badala ya siasa, akisema amechoka na silizo zilizo jaa uzandiki, futna majungu na mengine mengi.
Watu wakimsikiliza Ndg Lwakatare maarufu viunga vya bukoba kwa jina la Lwak's,'kifuba kya hitawa'katika hali ya bashasha na umakini.
Uwati mkubwa uliojitokeza kumsikiliza Lwakatare.



 Mapokezi ya Lwakatare uwanja wa ndege Mjini hapa.
Kasi ya kidedea cha mamia ya wafuasi wa Lwakatare waliojitokeza kumpokea uwanja wa ndege wa Manispaa ya Mji wa Bukoba.
Wakati  hali iko hivi Mjini BUKOBA IMERIPOTIWA kuwa Mahakama yaita  tena jalada la kesi ya Lwakatare
Mahakama ya Rufani imeiamuru Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuwasilisha mahakamani hapo majalada ya kesi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na mwenzake Ludovick Joseph Rwezaura.

Mahakama hiyo imeitisha majalada hayo, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha maombi ya marejeo mahakamani hapo dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu kuwafutia washtakiwa hao mashtaka ya ugaidi yaliyokuwa yakiwakabili.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza, zilisema tayari Mahakama ya Rufani imeshaiagiza Mahakama Kuu Dar es Salaam iwasilishe majalada hayo.

Msajili Kahyoza amesema baada ya kupokea amri ya Mahakama ya Rufani kuita jalada la kesi hiyo la Mahakama Kuu, nao wameiandikia barua Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuiamuru iwasilishe kwake jalada ya kesi hiyo. Lwakatare na Ludovick walikuwa wakikabiliwa na mashtaka manne.


Next Post Previous Post
Bukobawadau