Bukobawadau

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari muda huu amepigwa na kujeruhiwa vibaya damu zinamtoka Puani, amepigwa na vijana wa kisomali, katika eneo la Zaburi kata ya Makuyuni Jimbo la Monduli, Taarifa za awali zinasema baada ya Nassari kuondoka na gari jingine, waliokuwa wanafuatana naye walienda kujibanza sehemu. Kiongozi wa Chadema aliyetambulika kwa jina la Teddy Ndossi na dereva wa Nassari. Dereva wa Nassari Guardian Palangyo amepigwa mdomoni amevunjwa meno mawili, na kwa sasa wamempiga Katibu wa Chadema wa eneo hilo anayeitwa Kilongola, wapo Kituo cha Polisi Makuyuni kutafuta msaada zaidi. Picha na taarifa zaidi zitawajia baadae.

Next Post Previous Post
Bukobawadau