Bukobawadau

DK SHEIN AISUTA KAMATI YA MARIDHIANO

Nimekaa kimya takriban mwaka mmoja nimezuliwa ya kuzuliwa, yakasemwa yalosemwa nikaambiwa ya kuambiwa, nikashushwa hadhi yangu, nikagombanishwa na Chama Changu na Wazanzibar wenzangu.

Mimi Kamati ya Maridhiyano siijui.Wakanifata mimi Wazanzibar wenzangu sita ipo siku nitawataja majina yao.

Mmoja wao mkubwa wao wakaomba kuja kuniona, akazungumza na Katibu, sisi ndio Kamati ya Maridhiano na sisi ndio tuliofanya kazi kubwa ya Maridhiano wakasema tupo nikawaambiwa endeleeni.Wakaja mara ya pili kunipa pole.

Wakaja mara ya tatu sikuwaita waliomba nami nikawakubalia, wakanambia wamekuja wana mawazo ya kuzungumza kwenye mabadiliko ya katiba ya kuzungumza Muungano wa Makataba, nikawaambia msifanye haraka subirini tume ianze kazi yake nae mkatowe maoni yenu.

Hayo ni mawazo yenu si yangu kayasemeni ya kwenu na mimi nina msimamo wangu. Wakanambia tutakuwachia nakala usome wakanambia sisi tunakutengemea wewe nikawaambia mimi msinitegemee.

Makamo wa Pili naye aliporudi ziara yake Cuba nikamuuliza ushapewa nakala yako, akanambia hapana hakupewa, mimi nikampa yangu nikamwambia katoe kopi.

Wanasema mimi nishayabariki mawazo yao, mimi nimeyabariki lini? Sisi serikali hatuna maamuzi juu ya Katiba, mimi na Dkt. Kikwete hatuna msimamo juu ya Katiba Mpya.

Lakini sisi Chama cha Mapinduzi msimamo wetu ni serikali mbili. Wao waendelee na mambo yao mimi wasiniingize, mimi nina mambo yangu na CCM tuna mambo yetu. Nasema wasipande ndege yetu kwa sera zao.

Dkt. Shein aliyasema hayo jana jioni katika mkutano wa hadhara uloandaliwa na Chama Cha Mapinduzi. Huku akishangiliwa na wanachama wake alisema atapambana na CUF na sasa hakuna kulala.

“Wakifanya mkutani asubuhi tutafanya jioni, wakifanya mkutano jumamosi sisi tutafanya jumapili” alisema Dr Shein.


Next Post Previous Post
Bukobawadau