Bukobawadau

HABARI KWA MKUTASARI

Ndege ya kampuni ya Coastal inayofanya safari zake kutokea Dar kwenda kwenye miji na mapori karibu yote yenye airstrips hapa nchini ikiwa imebinuka huko Kiwanja cha ndege cha Arusha baada ya wahudumu wake kukosea namna ya upangaji wa mizigo ndani ya ndege hiyo na pia kutokuweka vifaa maalum vya usalama vya kuzuia kubinuka! Hili ni tatizo la kuchanganya Uswahili na mambo ya kitaalamu!-Picha kwa hisani ya PakaJimmy via JamiiForums
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia), akifafanua jambo kwa Mweyekiti wa Kampuni ya Alhayat Investment na Nembras Investment ya nchini Oman, Shekhe Salim Al-Harthy, wakati walipomtebelea ofisini kwake leo mchana. Kampuni ya Alhayat investment ni kampuni ambayo imeonyesha nia ya kuwekeza kwenye Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
 Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji mfanyabiashara, Bw. Marijani Abubakar 'Papa Msofe' akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam juzi, wakati akitoka kusomewa mashtaka ya mauaji yanayomkabili
Next Post Previous Post
Bukobawadau