Bukobawadau

LWAKATARE;POLISI MNACHEKESHA NA KUTIA AIBU!

Pamoja na kulazwa Muhimbili na shingo yangu kuuma,mikono yangu inafanya kazi. Katika waraka wangu wa 'Mrejesho toka Mahabusu Gerezani' niliouandika siku tatu baada ya kutoka gerezani Segerea iko sehemu niliyoandika kuhusu jeshi la polisi linaloongozwa na colledge mate wangu Said Mwema(IGP) kwamba kwa mfumo na weledi wanaoutumia kufanya kazi zao za kipolisi itawachukua karne nyingi kufaulu katika kazi yao ya kukamata wahalifu,na kwa kweli labda sasa niseme uwezekano huo naona hauwezekani kuwepo mpaka kiama kama tutaendelea kuogelea katika utaratibu tulionao sasa.
Kwa akili ya kawaida sana ambayo haijachakachuliwa kwa kiasi kikubwa,ningelikuwa na mamlaka yaleyale ya kipolisi yaliyotamka mbele ya vyombo vya habari na kuwaelekeza na kuwashauri viongozi wa madhehebu ya kidini kwamba upo umuhimu wa wao wenyewe kujitengenezea utaratibu wa ulinzi na kujilinda dhidi ya watu wanaowashambulia kwa mabomu,risasi,tindikali n.k na kwamba jeshi la polisi liko tayari hata kuwapa wakufunzi wa kipolisi ili kuwapa mafunzo na mbinu za kujilinda; kwa TAMKO la CHADEMA,la kuimarisha Red Brigade yetu kwa nia ya kujihami na vipigo vya Green Guard wakati wa chaguzi na mabomu yanayorushwa kwenye mikutano ya hadhara ya CHADEMA na kuwaua wanachama,kwa utaratibu uleule ulioelekezwa misikitini na makanisani hata kama ni kwa kujibalaguza pia ningeuelekeza utaratibu huohuo kwa viongozi wa CHADEMA na kuiweka milango yote ya polisi wazi tayari kutoa mashirikiano na usaidizi wa mafunzo stahili na sahihi kwa CHADEMA ili kudhibiti vitendo wanavyovilalamikia CHADEMA.
Kwa kauli zinazoendelea kutolewa na viongozi wa polisi hivi sasa dhidi ya matamko ya CHADEMA ni vituko na vichekesho kama siyo MAJANGA. Polisi ni kama wanapuliza vuvuzela la CCM na Green Guard yao bila aibu!!
IGP Mwema na wenzako,jifunzeni na uchaguzi wa marudio wa kata nne za Arusha ambapo Mwenyekiti wa TUME ya uchaguzi na jopo lake walipotinga wenyewe Arusha na kuwapiga 'STOP' Mkuu wa mkoa na RPC wake wasithubutu kuingilia uchaguzi huo, hakika hakuna mlio wowote wa risasi wala bomu vilivyosikika na uchaguzi kumalizika kwa usalama na bila hajizi, CCM kulambishwa 4 kwa 0! Matokeo haya ni aibu na fedhea kwa CCM na serikali yake na hakika wanastahili

kulaaniwa kwa vifo vyenye sura ya kisiasa na kigaidi vilivyokwisha tokea Arusha hadi sasa.
Wana-Arusha mnastahili pongezi , MKO NA MUNGU!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau