Bukobawadau

Familia ya Mandela yafungwa mdomo

RAIS Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini, ndiye mtu pekee atakayekuwa anatoa taarifa za maendeleo ya afya ya Rais wa kwanza mweusi wa nchini hapa, Nelson Mandela. Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao kilichoitishwa na Rais Zuma siku chache zilizopita na kuhudhuriwa na baadhi ya maofisa wa serikali ya Pretoria na mabalozi wa mataifa mbalimbali walioko nchini hapa.


Vyanzo vya habari vya Mtanzania kutoka ndani ya kikao hicho, vilidokeza kuwa kikao hicho kilikuwa cha kubadilisha mawazo lakini pia, Rais Zuma alikitumia kuwapa taarifa za hali ya afya ya Mandela na uamuzi wa serikali yake wa kuwa msemaji pekee wa suala hilo.

Mtanzania limedokezwa kuwa Rais Zuma aliwaambia mabalozi hao hali ya Mandela siyo nzuri bali ni mbaya.

Alisema Mandela anaendelea vizuri na matibabu kwa sababu dawa anazopewa zinaonyesha matumaini ya kumsaidia na kusisitiza kuwa bado yuko mahututi lakini imara.

Uamuzi mwingine uliopitishwa na serikali ni wa kuwazuia wale wote ambao wamekuwa wakifika hospitalini alikolazwa Mandela na kuomba kumuona kutokana na kuwa naye karibu wakati wa za ukombozi au kwa sababu nyingine,

Uamuzi wa sasa wa serikali kwa madaktari wa Mandela unawataka kutoa ruhusa kwa mkewe Graca Machel, watoto wake, wajukuu zake wanaoelezwa kutozidi sita na mtalaka wake, Winnie Mandela.

Habari nyingine zinasema Zuma, anatarajiwa kufanya mabadiliko mengine ndani ya serikali yake wiki hii yanayoelezwa kuwa yatawaacha kando wanasiasa wanaowaunga mkono wapinzani wake wa siasa.

Taarifa ambazo Mtanzania limezipata kutoka kwa makada wa chama

cha African National Union (ANC) zimeeleza kuwa Ris Zuma atafanya mabadiliko hayo kwa kuwaondoa kazini baadhi ya maofisa waandamizi wa serikali kabla ya Julai 18.
Next Post Previous Post
Bukobawadau