Bukobawadau

TASWIRA MKUTANO WA CHADEMA BUKOBA 15 JULAI, 2013 MAMA CONCESTA RWAMLAZA NA MH.WENJE WATOA ELIMU YA URAIA,MAMA CO

Mbunge wa Viti Maalumu ambaye pia ni katibu wa mkoa, Mama Concesta Rwamlaza akiongea na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Uhuru kusikiliza mkutanano wa M4C.
Mh.Ezekiel Wenje jukwaani akielezea namna CCM walivyoanisha kwenye waraka wao wa kupinga baadhi ya vifungu kwenye rasimu ya jaji Warioba ikiwa ni pamoja na CCM kung'ang'ania serikali mbili wakati ikitaka kulaghai wananchi kuwa kuwa na serikali tatu ni mzigo mkubwa kwa taifa. 

 Kushoto Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Bukoba ndg Shelejei
Amesema Tanganyika ina takribani mikoa 26 na hivo kila mkoa ukitoa wabunge wawili itakuwa na wabunge 52 na Zanzibar ina mikoa 10 hivyo wabunge 20 na wabunge 5 wa kuteuliwa na rais hivyo idadi ya wabunge haitazidi 80, kila nchi iongozwe na waziri mkuu na Tanganyika iwe na baraza la mawaziri lisilozidi mawaziri 7 pamoja rais kwa maana ya muungano na mawaziri wanaoshughulikia masuala ya muungano tu kwa kuwa ni machache. 

Akauliza wananchi upi ni mzigo mkubwa kati ya huo muundo amabao CDM wanaupendekeza na wa sasa ambao CCM wanautaka uendeleee wenye mawaziri 60 na wabunge takribani 446.

Vile vile akatolea ufafanuzi suala la RedBrigade na Green Guard; amesema anaunga mkono swala la kufundisha vijana ukakamavu kwa kuwa polisi na greenguard wanawaua na kuwajeruhi viongozi na wanachama wa CDM akitolea mfano kifo cha kiongozi wa CDM marehemu Msafiri aliyeuuwawa Usa-river Arusha, na kujeruhuiwa kwa Mbunge Machemli wa Ukerewe na Highness Kiwia mbunge wa Ilemela.

Mdau Valelia Mkurugenzi wa Vision Fm Radio akiwajibika
Katika hali ya usikivu  wanaonekana wadau


Mwisho Mh.Wenje kasema M4C itaendelea wilaya ya Muleba, Biharamulo, Geita-Nyang'wale. Sengerema.





M4C BUKOBA
Next Post Previous Post
Bukobawadau