Bukobawadau

Tendwa: Kwa hili la Red Brigade, Nitaifuta CHADEMA!

Hatimaye msajili wa vyama vya siasa Nchini John Tendwa ameibuka na kusema sasa anaandaa kalamu yake kukifuta Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.

Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari siku ya jana Tendwa amesema CHADEMA wanataka kuanzisha kikundi cha mgambo ambacho ni kinyume na sheria,katiba ya nchi na sheria za usajili wa vyama.

Msajili huyo ambaye inadaiwa ni mwanachama mwaminifu wa CCM amesema kwamba kama madai ya CHADEMA ni kuanzisha kikundi cha kujilinda dhidi ya Green Guard wa CCM madai hayo hayana msingi wowote kwani kama CHADEMA wana taarifa kwamba Green Guard wanahatarisha amani basi wanapaswa kuripoti suala hilo polisi ili lifanyiwe kazi kwa mujibu wa sheria.

Tendwa amezidi kuonya kwamba uamuzi wake ni wa mwisho na atakapoifuta CHADEMA maamuzi yake hayapingwi popote kisheria.

Tangu Kamati Kuu CHADEMA itoe tamko la kufundisha vijana wake ukakamavu kukabiliana na ukatili na uharamia unaofanywa na kikundi cha Green Guard ni kama Taifa limesimama na hiyo imekuwa ni habari kuu kila mahali.Dhihirisho linaloonyesha kwamba CHADEMA ndicho chama kinachofuatiliwa habari zake zaidi hapa nchini na pia kuwa na idadi kubwa zaidi ya watanzania wanaokiunga mkono.

Viongozi ambao wameshazungumzia Tamko hilo la CHADEMA ni Rais

Jakaya Kikwete,Jeshi la Polisi nchini,Viongozi wakuu wa CCM,Mwenyekiti wa NCCR James Mbatia na sasa Msajili wa vyama John Tendwa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau