Bukobawadau

MASHUJAA KUAGWA LEO 22 JULAI 2013

Na Mwandishi Wetu
MIILI ya askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa katika shambulio la kushtukiza katika Jimbo la Darfur, nchini Sudan itaagwa leo katika Viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi, Upanga, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi na baadaye kusafirishwa kwenda kwao kwa ajili ya maziko.Habari ambazo gazeti hili limepata, zimeeleza kuwa wanajeshi hao wataagwa kwa heshima zote za kijeshi na mara baada ya hapo, miili hiyo itasafirishwa kwenda kwao kwa ajili ya maziko. Wanajeshi waliouawa katika tukio hilo wakiwa katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (UN) mjini Darfur ni Sajini Shaibu Shekhe, Koplo Osward Paul Chaula, Koplo Mohamed Ally, Koplo Mohamed Chukilizo, Rodney Ndunguru, Fortunatus Msove na Peter Werema.

Miili ya wanajeshi hao iliwasili nchini jana na kupokewa kwa vilio, simanzi na huzuni kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki pamoja na viongozi wa kitaifa wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dkt. Mohamed Gharib Bilal.Ndege maalumu iliyobeba miili ya askari hao yenye namba B 737-400 Comb ZS-JRQ iliwasili jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One (Air Wing) saa 10.39.
A s k a r i h a o w a l i k u w a wakiwasindikiza waangalizi wa amani kutoka Khor Abeche kwenda mjini Darfur.Inaelezwa kuwa shambulio hilo lilitokea umbali wa kilomita 20 kutoka Makao Makuu ya kikosi hicho ambapo miongoni mwa waliojeruhiwa ni pamoja na maofisa na askari kutoka mataifa mengine.Wakati kikosi cha askari jeshi wa Tanzania kikishambuliwa, kilikuwa na askari 36 ambao ni miongoni mwa askari wanaolinda amani kwenye Kikosi cha UN mjini Darfur nchini Sudan
Next Post Previous Post
Bukobawadau