Bukobawadau

MSAJILI AIAGIZA MITANDAO KAGERA KUFANYA UCHAGUZI

Afisa maendeleo ya jamii mkoani Kagera, Charles Mwafimbo akiongea wakati wa kikao cha kutatua mgogoro uliopo kati ya uongozi wa KAGONET na mitandao ya wilaya inayoyaunganisha mashirka yasiyo ya kiserikali.
Msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali hapa nchini MICHAEL KATEMBA ameiagiza mitandao yote ya wilaya inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani KAGERA kuhakikisha inafanya uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi MITATU kuanzia sasa ili iweze kupata wawakilishi watakaoshiriki katika zoezi la kuwachagua viongozi wapya wataoongoza mtandaounaoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani humo (KANGONET).

Ametoa agizo hilo leo wakati wa kikao kilichowashirikisha wawakilishi wa mitandao inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kisekari toka katika wilaya zote zilizoko mkoani KAGERA kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya BUKOBA kilichokuwa na lengo la kumaliza mgogoro uliopo kati ya mitandao ya wilaya mkoani humo na uongozi wa sasa wa KANGONET.

Agizo alilolitoa KATEMBA limekuja baada ya kuelezwa na washiriki wa kikao hicho chanzo cha mgogoro ilioko kati ya uongozi wa sasa wa KANGONET na mitandao ya wilaya inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani KAGERA.

Katika kikao hicho wawakilishi wa mitandao ya wilaya kwa nyakati tofauti walimweleza , KATEMBA kuwa mgogoro ulipo kati ya mitandao wilaya na KANGONET kwamba unachangiwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa sasa ya kutaka kujinufaisha kupitia katika mtandao huo na kutokataka kuitisha mikutano na uchaguzi kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa KANGONET na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali (KADETFU) linalotuhumiwa kupora majukumu ya KAGONET, YUSTO MCHURUZA, katika kikao hicho amesema shirika lake la KADETFU kuwa halina mahusiano na mtandao wa KANGONET katika utendaji wake wa kazi, amesema mambo yanayoifanya KANGONET ishindwe kuitisha mkutano wa uchaguzi kuwa ni pamoja na ukata unaokabili mtandao huo.

Credit; Audax Kagera.
Next Post Previous Post
Bukobawadau