Bukobawadau

NI BAKWATA NA LOWASSA JIJINI MWANZA, MILIONI 590 ZACHANGISHWA KATIKA HARAMBEE.

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akiingia katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza, Pembeni kushoto ni Mdau Al Amin Abdul na kulia kabisa ni Mdau Hafidh Karugira(Nkurukumbi) 
 Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akipongezwa na kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al Badawikwa kumvika joho la kilemba  baada ya kufanikisha harambee kwa ajili ya Kituo cha Redio Ikra kinachomilikiwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza. 

Katika harambee hiyo zaidi ya sh. mil. 590 zilipatikana na kuvuka lengo ambalo lilikuwa sh. mil 500.

 WAZIRI Mkuu mstaafu  Mhe.Edward Lowassa ijumaa usiku aliongoza harambee kubwa  na ya kihistoria ya kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.
Anayeshuhudia ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Salum Hassan Fereji. 


 Mhe.Lowassa aliyekuwa Jijini Mwanza kushirikiana na marafiki zake, wafanyabiashara, taasisi na  makampuni mbalimbali, watu binafisi na viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wabunge wa majimbo mawili ya jijini Mwanza Ilemela na Nyamagana kupitia CHADEMA yaliyotuma wawakilishi wao hatimaye aliweza kuvuka lengo lililowekwa kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 590 zikiwemo ahadi.

Camera ikiangaza Kanda ya ziwa.
Next Post Previous Post
Bukobawadau