Bukobawadau

PINDA KUBURUTWA KORTINI ALHAMISI MASHTAKA YAKE TAYALI YAMEANDALIWA KAULI YA KIKWETE YAKWAMA KUMUOKOA

Na Mariam Mziwanda
KITUO c h a S h e r i a n a H a k i z a B i n a d a m u ( LHR C ) , k ime t a n g a z a kumburuta mahakamani keshokutwa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa kile kinachodaiwa amekaidi kufuta kauli yake ya kuruhusu vyombo vya usalama kupiga wananchi wanaokaidi amri za vyombo hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi na mwanasheria wa LHRC, Harold Sungusia, alisema wanamfungulia shtaka Waziri Mkuu Pinda, kesi ya kimkakati itakayomlazimu ajibu mbele ya mahakama msimamo wa Serikali iliyosababisha atoe kauli hiyo.
Katika kikao cha Bunge lililopita wakati wa maswali ya papo kwa papo Waziri Mkuu alisema;“Ukifanya fujo na umeambiwa usifanye hiki na wewe ukaamua ukakaidi utapigwa tu, maana hakuna namna nyingine...ehee maana wote tukubaliane nchi inaongozwa kwa misingi ya kisheria, sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona wewe ni imara zaidi, wewe ndiyo jeuri zaidi watakupigwa tu na mimi nasema muwapige kwa sababu hakuna namna nyingine maana tumechoka sasa.”
Sungusia alisema kauli hiyo ya Waziri Pinda ni uvunjaji wa katiba ya nchi na haki za binadamu, hivyo hawataikalia kimya. Alisema walishamtaka afute kauli yake, lakini hakufanya hivyo.
Alisema pamoja na bosi wake (Rais Jakaya Kikwete) kueleza umma kuwa Waziri Pinda, aliteleza, lakini bado LHRC inaona anayo ya kujibu mbele ya mahakama.
Mwanasheria huyo alifafanua kuwa kauli ya Waziri Pinda ni ukiukaji wa ibara ya 13 ya sheria inayozungumzia usawa mbele ya sheria na ibara ya 30 ibara ndogo ya (3) inayoeleza kama haki ya mtu inavunjwa, imeshavunjwa au inaelekea kuvunjwa unaweza kupeleka shauri lako Mahakama Kuu.
“Kwa hiyo LHRC hatutamvumilia na kuona haki za raia zinavunjwa... kauli ya Pinda ametudhihirishia msimamo wa Serikali, hivyo hata waliokuwa wanafanya matukio na kunyanyasa raia (polisi) kumbe walikuwa mgongoni mwake na walikuwa wakilindwa na yeye,” alisema Singusia.
Kuhusu ripoti ya nusu mwaka ya kituo hicho, LHRC iliainisha vifo vya wananchi vilivyosababishwa na vyombo vya sheria. Kwa mujibu wa takwimu hizo, kwa mwaka huu kati ya Januari hadi Juni watu 22 wamekufa kwenye mikono ya polisi, wanajeshi ama Sungusungu.
Kwa upande wa Katiba, Singusia alisema vyama vya siasa vinatakiwa kukaa pembeni kuwaachia wananchi suala zima la rasimu ya katiba ili kuepuka kuwa na Katiba iliyopatikana kwa matakwa ya vyama hivyo ambayo yatakuwa si maamuzi ya wengi kwani idadi kubw ani watu wasio na chama nchini.
Alisema kutokana na umuhimu huo wa mchakato wa katiba ni vyema suala hilo likaendeshwa kwa umakini ili ipatikane katiba itakayokidhi matakwa ya wengi, kwani bado maeneo ya vijijini na pembezoni mwa nchi watu wengi hawakupata nafasi ya kutosha ya kutoa maoni yao.
Kituo hicho pia kimeishauri Serikali kuona umuhimu wa kuwepo kwa sera ili kuwa na sheria itakayozungumzia suala la imani za ushirikina.
Alisema hiyo ni kwa sababu watu wengi wanakufa kutokana na imani hizo. Alisema hadi Juni mwaka huu watu 300 waliuawa kwa imani za aina hiyo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau