Bukobawadau

SIMULIZI KUTOKA KWA MDAU ASIIMWE.

Lilitolewa tangazo kuwa familia yoyote yenye Watoto kumi wa kuzaliwa katika familia hiyo. itapata million kumi za kuisaidi kuwatunza Watoto hao.

Aliyesikia tangazo hilo ni baba. Pale nyumbani walikuwa na Watoto tisa, akakumbuka kuwa alipata Mtoto Nje ya ndoa akamtelekeza! Akaona sasa huu ndiyo muda muhafaka wa kwenda kumtafuta mtoto wake wa nje ya ndoa ili afikishe idadi ya Watoto kumi, aweze kupewa million zake kumi.

Siku zote alikuwa anashindwa kumueleza ukweli mke wake, lakini kwa sababu ya kutaka kuondokana na umasikini akasema potelea mbali, liwalo na liwe leo lazima niweke mambo bayana.
Baada ya kueleza habari nzima, baba hakuamini masikio yake alipoambiwa kwa upole kuwa siyo neno! Mwenye makosa husamehewa!

Yule baba alitimua mbio kwenda kumtafuta yule Mtoto aliyemtelekeza, bila kujali siku zote huyo Mtoto alikuwa anakula nini! Kule nako hakupata shida kwa sababu ilionekana ni heri! Sasa Mtoto kawa Mtoto sawa na wengine.
Aliporudi nyumbani alimkuta mke wake peke yake! Alipouliza Watoto wengine wako wapi alijibiwa kuwa, kosa siyo kosa bali kosa ni kurudia kosa! Akasema kuwa hatarudia tena.
Baba akauliza kwani kulikoni?...Mama akajibu kwamba wale Watoto wote tisa wote wamechukuliwa kama yeye alivyokwenda kumchukua wa kwake!

Credit;Mdau Asiimwe.
Next Post Previous Post
Bukobawadau