Bukobawadau

WANYAMBO SIO WAHAYA KAMA INAVYOSADIKIKA

Moja ya ngoma asilia za wanyambo wa Karagwe- Amakondere.

Tamasha la utamaduni wa Kabila la Wanyambo waishio katikaWilaya za Karagwe na Kyerwa Mkoani Kagera, limeshuhudia maelfu ya washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya hizo kutoka kwa mwenzake kuhusiana na mila na desturi asilia za kabila hilo ,mila zao ambazo zinazidi kutoweka kila uchao, kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kuenea kwa Teknolojia mpya zinazoibuka zikieneza tamaduni za kigeni kutoka maeneo mengine hasa kutoka nchi za ughaibuni.Kubwa zaidi wanyambo walikuwa na hamu ya kujua ni kwa nini kabila lao linafananishwa na lile la ndugu zao Wahaya kutoka Bukoba.

Taasisi zinazojishughulisha na uhamasishaji wa utamaduni asilia,vikundi vya ngoma asilia vya vijana na wazee,wakishirikishwa watoto kwa uchache,wakiongozwa na shirika la SAWAKA ambalo limeshiriki kuratibu Tamasha hilo Wilaya za Karagwe na Kyerwa,walijimwaga katika uwanja wa mpira wa miguu mjini Kayanga ambako lilifanyika tamasha hilo, likizihusisha Wilaya hizo mbili ambazo asili yake ni moja kwa kuunganishwa na kabila moja la Wanyambo wote wakijitahidi kutetea kabila hilo.

Akisoma Historia ya Karagwe tangu enzi za utawala wa Wakama, historia iliyosheheni chimbuko la kabila hili ambalo kiukweli limefichika ndani ya Kabila la wahaya, ukiuliza kabila la mkazi wa Karagwe nje ya mkoa wa Kagera kwa walio wengi, Mratibu wa Shirika la SAIDIA WAZEE KARAGWE (SAWAKA)ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirika la KARAGWE MEDIA ASSOCIATION (KAMEA)Shirika ambalo ni mmiliki wa Radio Karagwe FM Bw.Livingiston Byekwaso amesema kuwa,asili ya jina Karagwe kutokana na simulizi za wazee mbalimbali na watafiti wa historia ya Karagwe akiwemo Profesa Katoke katika kitabu chake alichokitunga mwaka 1975,inaelezwa kuwa ,jina hili lilitokana na kilima kilichoko kusini Magharibi mwa makao makuu ya Wilaya ya Karagwe kwenye kijiji cha Kandegesho Kata ya Nyakakika mahali ambako Mukama wa Kwanza Nono ya Marija alifanyia kafara ya kwanza.

Akiendelea kuelezea umuhimu wa kuuenzi utamaduni wa mnyambo ambao umekuwa haujulikani, Byekwaso alisema.“ Kwa tafsiri yangu napenda kuamini kwamba,wakoloni kwa sababu ya kurahisisha utawala walilinganisha wanyambo toka Karagwe na Wahaya kutoka Bukoba na wote kuitwa Wahaya, ili kurahisisha utawala wao walipoingia hapa nchini.Lakini ni ukweli usiopingika kwamba wanyambo wanapatikana katika Wilaya ya Karagwe na wahaya kutoka Bukoba wanatofautiana sana kutokana na asili yao,shughuli za kiuchumi,kijamii,mila na desturi,mazingira na lugha zao”.

Akiwahutubia washiriki wa Tamasha hilo,mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe Mustafa Said alisema kuwa,Utandawazi umekuwa changamoto kubwa ambapo vijana walio wengi wamejikita katika mitandao ya kijamii kama vile facebook ,twitter na mitandao ya kisasa jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kusababisha mmomonyoko wa maadili ya utamaduni asilia.Saidi aliwataka vijana kuwa makini na matumizi ya utandawazi kwani utandawazi huo ukitumika vibaya,madhara yake ni makubwa
.Aidha aliwataka wana Karagwe kuziepuka mila na desturi potofu hasa tabia za wanaume kuwachapa viboko wanawake zao.
CREDIT BUKOBAWADAU VIA RADIO GARAGWE
Next Post Previous Post
Bukobawadau