Bukobawadau

Alex Massawe afunguliwa kesi ya kughushi • MAHAKAMA YAAMURU AREJESHWE NCHINI

na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imetoa hati ya kukamatwa na kurejeshwa nchini mfanyabiashara maarufu nchini, Alex Massawe, ili aje kukabiliana na kesi yake mpya ya kughushi nyaraka za umiliki wa ardhi na kutoa taarifa za uongo.
Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi, Gene Dudu, muda mfupi baada ya wakili Mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kuwasilisha ombi hilo mahakamani akiarifu kuwa upande wa jamhuri umemfungulia Massawe kesi na.150/2013 ya kughushi hati za umiliki wa ardhi na kutoa nyaraka za uongo mahakamani hapo.
Massawe ambaye anashikiliwa na askari wa Interpol Dubai, hakuwepo mahakamani hapo wakati kesi hiyo ikifunguliwa.
Hakimu Dudu alisema anakubaliana na ombi hilo la Kweka na kwamba mahakama yake imetoa amri ya kukamatwa kwa Masawe kokote aliko na arejeshwe nchini ili aje akabiliane na kesi yake hiyo mpya iliyofunguliwa mahakamani hapo.
Aidha Hakimu Dudu alisema pia anakubaliana na ombi la wakili Kweka lililokuwa linaiomba mahakama hiyo itamke majina sahihi yanayotumiwa na Massawe kwa kuwa kule Dubai anakoshikiliwa na askari wa Interpol anatumia majina mengi.
Alisema majina halali ya Massawe ni Alex Siliyamala Massawe ambayo ndiyo yaliyoandikwa kwenye hati ya mashtaka ya kesi hiyo Na.150 ya mwaka huu.
Hivi karibuni vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Interpol cha Jeshi la Polisi hapa nchini, Babile, alivithibitishia vyombo vya habari kuwa Massawe amekamatwa na askari wa Interol huko Dubai kwa tuhuma mbalimbali.

Next Post Previous Post
Bukobawadau