Bukobawadau

HII NDIYO NDEGE ILIYOLAZIMIKA KUTUA ZIWA LA MANYARA BAADA YA INJINI MOJA KUFELI

Ndege Ndogo ya Shirika binafsi la Ndege la TANZANAIR iliyokuwa ikitokea Mjini Bukoba kuelekea Jijini Dar es Salaam kupitia Zanzibar, imelazimika kutua katikati ya Ziwa Manyara lililopo Mkoani Arusha ili kunusuru abiria wake sita (6) waliokuwamo katika ndege hiyo baada ya kupatwa na hitilafu kwa kuzima ghafla kwa Injini moja wakati ikiwa hewani. Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Kamanda Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa ajali hilo majira ya saa 2.35 asubuhi maeneo ya Lambi, kusini mwa wilaya ya Babati.
Next Post Previous Post
Bukobawadau