Bukobawadau

BUKOBA YETU NA CAMERA YETU LEO 30 AGOSTI,2013.

Muonekano wa jengo la New Banana hotel, moja kati hotel  zilizopo mjini Bukoba iliyojipatia umaarufu mwishoni mwa 80's ,ingawa ni yazamani  hadi hivi sasa inaendelea kufanya vyema.
Ndani ya New Banana hotel, nikiwa na Mzee wetu Haji Abbakari Galiatano,katika kufurahi siku na kubadilishana mawazo ,ingawa umri wake ni mkubwa lakini mawazo yake bado ni chachu kulingana na kasi iliyopo.Bukobawadau Blog tunamuombea kwa mwenyezi mungu azidi kumjalia na kumpa nguvu zaidi.
 Usambazaji wa sukari inayo zalishwa na kiwanda cha Kagera Sugar kilichopo Wilayani Missenyi.Wilaya yenye Tarafa 2, Kata 17, vijiji 74 na vitongoji 351. Kuna jimbo moja la uwakilishi Bungeni (Nkenge); Wilaya ina Madiwani 23 na Mbunge 1, kati ya madiwani hao 17 ni wa kuchaguliwa kutoka kwenye Kata na 5 ni kutokana na Viti Maalum.
Kwa mujibu wa tovuti ya mkoa Kiwanda cha Sukari Kagera (Kagera Sugar Limited) Sera ya Ubinafshaji imesaidia kufufuliwa kwa Kiwanda hiki ambacho kilisimamisha uzalishaji wake miaka saba (7) iliyopita. Mashamba ya miwa yenye ukubwa wa ekari 9500 yamelimwa na miundo mbinu ya Kiwanda imefufuliwa na kujengwa upya. Upanuzi wa mashamba bado unaendelea hadi lengo la ekari 20,000. Kiwanda kimeanza uzalishaji wa Sukari mwishoni mwa Oktoba, 2007. Hadi sasa Kiwanda kimetoa ajira kwa Watanzania katika fani mbalimbali wapatao 700 na pia hutoa ajira kwa wafanyakazi 1,300 kwa kazi za kutwa kila mwezi.
Mitaa ya Dollas hotel.
Muonekano wa jengo la Rwabizi kushoto, kulia ni kasi ya muekezaji mwingine ikiendelea.
Camera yetu uso kwa uso na wadau pichani, kutoka kushoto ni Mzee Kaizilege  Diwani wa zamani kata ya Rwamishenye , kulia ni Haji Sadick Galiatano,ni wadau wa kwanza kabisa kukutana na Bukobawadau tukiwa katika kuchukua maoni  juu ya mstakari wa kisiasa na yale yanayoendelea ndani ya manispaa ya Mji wa Bukoba.

Heka heka zikiendelea katika vibanda vilivyopo nje ya soko kuu mjini Bukoba.
Anaitwa Athmani Bahati mfanyabiashara wa Vifaa vya umeme anapatikana barabara ya Arusha nje ya Soko kuu Bukoba ni mfatiliaji wa mambo mbalimbali kijamii, kisiasa na kiuchumi(kwa sababu zake binafsi)

Next Post Previous Post
Bukobawadau