Bukobawadau

Sikiliza Mjadala juu ya madawa ya kulevya Tanzania.

Katika mjadala wetu tunazungumzia suala la tatizo la biashara haramu ya madawa ya kulevya nchini Tanzania kwa mujibu wa takwimu mbali mbali ni kwamba watanzania wapatao 240 baadhi yao wakiwa wasanii wameshakamatwa katika nchi mbali mbali duniani wakiwa na madawa haya yenye thamani ya mabilioni ya shilingi. Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ameshaalika baadhi ya waathirika Ikulu akiwamo mmoja wa wasanii maarufu nchini humo Ray C katika juhudi za kupambana na matumizi ya madawa hayo. Katika mjadala huu tulikuwa mkuu wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya nchini Tanzania Godfrey Nzowa , mbunge wa Chadema (viti maalum) mjini magharibi Mariam Msabaha na Meneja wa Trent Recovery nyumba ya kusaidia watu wanaotumia madawa Zanzibar na mtumiaji wa zamani. Abdu Rahman Abdallah. Kusikiliza mahojiano mjadala huo bofya hapa. VIA VOA.
Next Post Previous Post
Bukobawadau