Bukobawadau

Rais Billy Clinton avitembelea vikundi chini ya taasisi yake TZ

Rais wa zamani wa Marekani Bw. Bill clinton amefanya ziara ya kukagua moja ya vikundi ambavyo vimekuwa vikifadhiliwa na taasisi yake ya clinton foundationi kwa ushirikiano wa shirika la kimataifa la plan,care na barclays ambapo amejionea shughuri mbalimba zinazofanywa na kikundi hicho cha upendo hisa Group kilichopo Mtambani Vingunguti jijini Dar es salaam .

Akizungumza mara baada ya kushuhudia shughuli mbalimbali zinazo endeshwa na kikundi hicho ikiwemo kutembelea miradi inayofanywa na wanakikundi hao clintoni amesema ameridhishwa na mpango huo unavyoendeshwa ambapo amewapongeza wanakikundi hao kwa jitihada zao wanazo zifanya katika kujiletea maendeleo wao binafi mbali na mkopo waliopatiwa kupitia mpango
Wakizungumzia mpango huo mshauri wa masuala ya biashara wa shirika la plan na mkuu wa wawafanyakazi ofisi ya mtendaji mkuu wa barclays wamesema mpango wa "banking on change" ambao umelenga kuwasaidia watu masikini umetekelezwa hapa nchini kwa muda wa miaka 3 ambapo mpaka sasa umesha wafikia watu 60 huku asilimia 80 wakiwa ni wanawake na kufafanua kuwa mpango huo utaendelea tena kwa miaka 3 ambapo katika kipindi hicho mpango huo umelenga zaidi kusaidia kundi la vijana.

Akiwa katika eneo hilo Bw Clinton alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya mitaa ya eneo hilo na kusalimiana na wananchi mbalimbali waliojitokeza kushuhudia tendo hilo
Next Post Previous Post
Bukobawadau