Bukobawadau

NAPE;Kipigo cha ZANU-PF dhidi ya MDC Zimbabwe ni salaam tosha!

Kipigo cha MDC Zimbabwe na ushindi wa kishindo wa Mugabe ni salaam tosha kwa wapinzani nchini jinsi wanavyoendesha siasa na kujenga matumaini yasiyokuwa na msingi wa kweli.

Ukiangalia kampeni zilivyokwendana matumaini waliyokuwa nayo MDC na wafuasi wao, hakika ndoto za mchana zinaua upinzani Afrika.

Nilisikia kauli kwa mfano Mzimbabwe mmoja alisema "watu wameichoka ZANU-PF,watu wanataka mabadiliko, MDC itashinda"! Akamalizia kwa kuchagiza "nguvu ya umma"!

Coln.(rtd) Kinana mzoefu wa kuongoza kampeni za CCM nchini toka 1995 mpaka 2010 aliwahi kusema "nguvu ya umma kwenye box la kura sio kelele za barabarani"!

Ni vizuri kujitathimini kwa vigezo sahihi kuliko kujifariji kwa vigezo vya kujifurahisha!
NINA AMINI UIMARA WA UPINZANI NCHINI SI TU NI WA FAIDA KWA NCHI BALI NI WA FAIDA HATA KWA CCM YENYEWE!

Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity
Next Post Previous Post
Bukobawadau