Bukobawadau

SAKATA LA MADIWANI BUKOBA HII NI KAULI YA NAPE KUPITIA JF;'Masilahi ya Wananchi na Nchi kwanza ya Chama baadae!'

Kumekuwa na mijadala kadhaa juu ya namna mambo yanavyokwenda ndani ya CCM hasa kufuatia sakata la madiwani na Meya wa Manispaa ya Bukoba. Kimsingi hali si tete kama inavyojaribu kuelezwa. Taratibu, kanuni, sheria na Katiba ya Chama kupitia vikao vitatumika kulimaliza swala hili kwa amani kabisa. Mwisho wa siku lazima wananchi wa Bukoba na Manispaa yao wapate haki yao ya msingi!

Nimewahi kusema siku nyingi kidogo kuwa NCHI KWANZA VYAMA BAADAE! Tafsiri rahisi hapa ni kuwa masilahi ya wananchi na nchi yao kwanza, masilahi ya Chama na itikadi zetu baadae!

Hivyo kwa kifupi kwa swala la Bukoba lazima masilahi ya wananchi wa Bukoba yatangulizwe mbele na yavuke ushabiki wa kiitikadi. Hatuwezi kupofushwa na mapenzi kwa vyama vyetu tukafumbia macho masilahi mapana ya wanachi wa Bukoba!

Hii haimaanishi sikipendi Chama changu bali ukweli ni kuwa naipenda sana CCM yangu lakini naipenda zaidi nchi yangu!
Mungu ibariki nchi yangu nzuri ya Tanzania
Mungu ibariki CCM iwahudumie vyema Watanzania!
Nape Nnauye
Next Post Previous Post
Bukobawadau