Bukobawadau

TAARIFA ZISIZO SAHIHI NI HATARISHI KWA AMANI NA USTAWI WETU KAMA TAIFA

Ukipokea UJUMBE au Taarifa zisizo na UTHIBITISHO FUTA DELETE KABISA 

Ninaamini watanzania watafaidika zaidi na matumizi mazuri ya mawasiliano. Ninaamini pia matumizi mabaya ya mawasiliano, ikiwemo mitandao ya kijamii sio tija. Tutumie mawasiliano vizuri.

Tutumie mitandao ya kijamii kwa maendeleo. Ukipokea ujumbe wa chuki, matusi, uchochezi, udhalilishaji wa mwanamke, mtoto au mwanaume, FUTA DELETE KABISA. au ignore/puuzia, usisambaze kwa wengine.

Tushiriki majadiliano kwa nia njema, tusitukanane, tujibizane hoja kwa hoja, matusi sio sehemu ya hoja.

Kama Admin nitusimamia vizuri majadiliano ili kuboresha matumizi mazuri ya jukwaa hili.

Tusiingilie uhuru wa watu kujieleza, tuutumie uhuru kutoa maoni yetu kwa uhuru tukizingatia uhuru wetu unakutana na uhuru wa wajihi wa wengine!..
Next Post Previous Post
Bukobawadau