Bukobawadau

TASWIRA WANAWAKE WAJASIRIAMALI WA BANDARI YA BUKOBA WAKITOA SHUKRANI KWA BALOZI HAMIS KAGASHEKI

Balozi Hamis Kagasheki akiongea na umoja wa wanawake wajasiriamali  wa ndizi katika bandari ya bukoba ambapo Mh Kagasheki amewalipia chumba cha ofisi kodi kwa mwaka mzima na kuwapatia pesa ya nyongeza kiasi cha milioni 2.
Sehemu ya Wanawake wajasiriamali wa ndizi katika bandari ya Bukoba walio mualika Balozi Hamis Kagashek(Mbunge jimbo la Bukoba Mjini)kwa lengo la kumshukru kwa msaada wa pesa na mawazo aliyowapa mwaka 2010 na hivi sasa wameanzisha umoja wao wa kukopeshana.Katika picha ya pamoja baada ya kupokea milion 2 na pesa ya kulipia kodi ya ofisi  pia Balozi kagasheki amesisitiza hakuna shughuli bila kuwa na ofisi.Bukobawadau blog tunatoa shukrani kubwa kwako Balozi Kagasheki.
Kaka Mkubwa akitoa angalizo

Kila mdau na uso wenye furaha.

Mkuu wa bandari akitabasamu baada ya kupewa zawadi ya kitambaa cha suti ikiwa ni asante kutoka kwa umoja wa wanawake hao.

Mkuu wa Bandari ya Bukoba nae akitoa neno juu ya umoja huo maana amekuwa mtu wa karibu sana na wafanyabiashara hao kimawazo na kuwaeleza ili na lile katika kuimarisha umoja huo.Pamoja na furaha kubwa kina mama hao walitoa shukrani ya mdomo na wakampa Balozi zawadi ya mbuzi kama heshima ya kitoweo na kitenge cha mama Kagasheki(Mke wa mbunge) pia kitambaa cha suti ili aendelee kuwa nadhifu kama kawaida yake.
Zawadi zikipokelewa.
Pichani anaonekana Mdau Sued Juma Kagasheki akiwa na mbuzi mnyama.Picha kwa hisani ya Jamco.
Next Post Previous Post
Bukobawadau