Bukobawadau

Malinzi ajitosa tena urais TFF


Dar. Jamal Malinzi na Omari Musa Nkwarulo ni miongoni mwa watu 25 waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Fomu hizo zilianza kutolewa juzi, ambapo waliochukua fomu za kugombea urais ni Jamal Malinzi na Omari Musa Nkwarulo wakati umakamu wa rais hadi sasa umewavutia Wallace Karia na Ramadhan Nassib.
Waliochukua fomu za ujumbe ni Athuman Kambi, Charles Komba, Davis Mosha, Elias Mwanjala, Eliud Mvella, Epaphra Swai, Farid Nahdi, Hussein Mwamba, Jumbe Magati, Kamwanga Tambwe na Khalid Mohamed.
Wengine ni Muhsin Balhabou, Omari Abdulkadir, Omari Walii, Samwel Nyalla, Shaffih Dauda, Stanley Lugenge, Twahir Njoki, Vedastus Lufano, Venance Mwamoto na Wilfred Kidao.
Kwa upande wa Bodi ya Ligi Kuu aliyechukua fomu mpaka sasa ni Hamad Yahya anayeomba kuteuliwa kugombea nafasi ya uenyekiti.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni saa 10 kamili jioni ya Agosti 20, mwaka huu
Next Post Previous Post
Bukobawadau