Bukobawadau

OPERESHENI KIMBUNGA YAANZA KWA MAFANIKIO MAKUBWA WAHAMIAJI HARAMU, MAJAMBAZI NA SIRAHA VYAFICHULIWA

 Mhe. Massawe na Kamanda Simon Sirro Msaidizi wa Kamanda wa Operesheni Kimbunga Wakiongea na Waandishi wa Habari
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe Katikati Akisistiza Jambo kwa Waandishi wa Habari
  Hivi ni Vyombo vya Habari Kwa ajili ya Kuwajulisha Wananchi nini Kinaendelea na Wazee wa Kazi Wakiwa Kazini
 Waandishi wa Habari Wakiwa Kazini Wakati wa Kupata Habari Juu ya Operesheni Kimbunga
Huu ni Mfano wa Picha ya Baadhi ya Aina za Siraha Zinazotumiwa na Majambazi Kuteka Wananchi na Mali zao  Nchini

Operesheni kimbunga ya kuwasaka wahamiaji haramu, majambazi na siraha za kivita imeanza kuonyesha ufanisi mkubwa baada ya siku mbili kuanza tayari wahamiaji haramu 1850 wametiwa mbaloni, siraha 7 zimekamatwa, na ng’ombe 1765 zimekamatwa katika mapori ya akiba.
Taarifa hiyo ilitolewa katika mkutano wa waandishi wa habari Jumapili tarehe 8/09/2013 na Kamanda Simon Sirro Mkuu wa Operesheni za Polisi nchini ambaye ni msaidizi wa Kamanda wa Operesheni  Kimbunga  ya kuwasaka wahamiaji haramu, siraha na majambazi katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Kamanda Sirro alisema operesheni hiyo ilianza tarehe 6/09/2013 na kufikia tarehe 8/09/2013 katika Mkoa wa Kagera wahamiaji haramu waliokamatwa ni 750, bunduki (magobole) 2, na ng’ombe 1323. Mkoa wa Kigoma wahamiaji haramu 855, Bunduki 2, na ng’ombe 200.
Pia katika mkoa wa Geita wameishakamatwa wahamiaji haramu 246, Bunduki magobole 3, ng’ombe 240 sare moja ya  Jeshi la wananchi Tanzania.  Ng’ombe walikamatwa katika mapori ya akiba ya Moyovosi Kigoma, Burigi Kagera (Karagwe na Kyerwa) na maeneo mbalimbali ya mkoa wa Geita.
Katika hatua niyingine Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Kanali Mstaafu Fabian Massawe alisema  tarehe 26/07/2013 baada ya Rais Kikwete kuagiza  wahamiaji haramu kuondoka kwa hiari na majambazi kujisalimisha na siraha  zao kabla ya operesheni kimbunga, walioondika kwa hiari ni 11,601.
Aidha siraha zilizosalimishwa ni 65 (SMG 3, Shortgun 10, Magobole 52) na siraha hizo nyingi zilipatikana katika wilaya ya Biharamulo. Pia Mhe. Massawe alisema ilitarajiwa waondoke wahamiaji haramu 52,000 mpaka 53,000 lakini mpaka operesheni inaanza waliondoka 11,601 na wengi kubaki nchini.
Angalizo, Kamanda Sirro alitoa angalizo na kuonya wanananchi watakaogundulika kuwaficha wahamiaji haramu kuwa  watachukuliwa hatua kali za kisheria, pia jambazi yeyote atakayetaka kutumia siraha kujihamia atakiona cha moto kutoka vyombo vya ulinzi na usalama vinavyoondesha operesheni hiyo.
Pia Kamanda Sirro aliwahakikishia wananchi kuwa operesheni kimbunga hiyo itazingatia haki za binadamu na hakuna mtu yeyote atakayeonewa wala kunyanyaswa au kunyanganywa mali zake kwa nguvu.
Imeandikwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013
Next Post Previous Post
Bukobawadau