Bukobawadau

*Wadau wa muziki wamfagilia hafsa kazinja kwa kumuenzi muhidin maalim gurumo*

Malkia wa Zouk Hafsa Kazinja ameendelea kujizolea sifa toka kwa wadau wa muziki ndani na nje ya nchi baada ya kutoa wimbo wa NIMUOKOKE NANI Remix kama njia ya kumuenzi mkongwe Muhidin Maalim Gurumo aliyestaafu rasmi kazi ya muziki. *Ngoma hiyo, iliyotengenezwa studio za OM Production chini ya wakali wa muziki wa dansi Omari Mkali na Abdul Salvador na ambayo imeanza kutamba katika vituo vya redion, inawakumbusha watu wazima miaka ya 70 wakati Gurumo alipotoa wimbo huo wenye kitenmdawili ambapo sasa vijana ambao ndio mwanzo wanausikia wameanza kukijadili kitendawili hicho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau