Bukobawadau

Bi. Jacqueline M. Maleko ateuliuwa kuwa mkurugenzi mkuu wa TANTRADE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi. Jacqueline M. Maleko (pichani kulia) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo ulianza Septemba 10, mwaka huu, 2013. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Maleko alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Masoko, Wizara ya Viwanda na Biashara, kabla ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, *Ikulu*.DAR ES SALAAM
Next Post Previous Post
Bukobawadau