Bukobawadau

Mjumbe wa NEC ya CCM akamatwa kwa ujangili

OPERESHENI Okoa Maliasili inayoendelea Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma imemkumba Mjumbe wa mkutano Mkuu wa CCM taifa (Mnek) Sultani Ajili Kalolo na kuhojiwa kwa zaidi ya Masaa 8 kwa tuhuma za kushiriki katika vitendo vya ujangili wa Tembo.

Tukio la kukamatwa kwa Mneki huyo lilitokea Oktoba 13 mwaka huu huku Wilaya hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kukamatwa kwa Bunduki zaidi ya 300 na Risasi 667 katika oparesheni hiyo ya okoa maliasili iliyobatizwa jina la “wazee wa tinted”.

Katika tukio hilo Mjumbe huyo wa mkutano Mkuu wa CCM taifa (Mnek) Ajili Kalolo alikamatwa akiwa Nyumbani kwake eneo la Shule ya msingi Muungano majira ya asubuhi na ilipofika saa 12 jioni Kikosi kinachosimamia operesheni hiyo kiliwaruhusu ndugu zake kumdhamini kwa masharti ya kwenda kuripoti kituo cha Polisi Jumatano ya wiki hii.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedith Nsimeki pamoja na kudai kuwa yeye siyo msemaji wa Operesheni hiyo Iakini alikiri kuwepo kwa tukio hilo la kukamatwa kwa Kalolo na kuongeza kuwa watu wanaokamatwa ni waliohusika katika matukio ya ujangili pamoja na madalali wa biashara ya meno ya Tembo.

“unajua mimi siyo msemaji wa Operesheni hiyo, lakini ninazo taarifa za Kushikiliwa kwa muda kwa kiongozi huyo wa ngazi za juu katika Chama cha Mapinduzi” alisema Kamanda Nsimeki na Kuongeza kuwa hali hiyo imetokana na Kiongozi huyo kutanjwa kuwa ni miongoni mwa Majangili wa Tembo.

“opereshini hii inatekelezwa kisheria, hivyo haiwezi kumuonea aibu kiongozi ama mtu maarufu” alisema kamanda Nsimeki na kuongeza kuwa watu wote wanaokamatwa ni wale wanaotajwa kuwa miongoni mwa wahusika wa namna moja na matukio na vitendo vya kijangili hivyo operesheni hiyo haitawaonea watu wasio husika.

Kamanda Nsimeki aliendelea kueleza kuwa Operesheni hiyo iliyopewa jina la okoa maliasili inayoendelea Wilayani Tunduru, Mkoani Ruvuma pia inaendelea katika Wilaya ya Namtumbo katika Kijiji cha Likusenkuse na Lipalamba Wilayani Mbingalengo likiwa ni kukomesha vitendo vya ujangili wa Tembo na maliasili nyingine za Tanzania.

Alisema Operesheni hiyo inayo husisha Vyombo mbalimbali vya Majeshi ya nchi yetu, wamo pia Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzani, Usalama wa taifa, Uhamiaji na Polisi ambao kwa pamoja wanapitia taarifa mbalimbali na kuwakamata watu wote ambao wamekuwa wakitajwa kujihushisha na matukio ya ujangili.

credit: Tabianchi blog
Next Post Previous Post
Bukobawadau