Bukobawadau

ADAPT OR DIE

Adapt or die

Inashangaza sana kwenye mahusiano, mtu anajua kabisa kuwa kila mmoja ametokea kwenye mazingira, malezi au makuzi tofauti. Maisha na “backgrounds” zetu zinatofautiana, jinsia zetu halikadhalika na kwahiyo tabia kutofautiana sio kitu cha ajabu, kwanza msipotofautiana tutawashangaa. Kama kutofautiana kwa tabia na mitazamo kupo basi suala la kubadilika na kubadilisha tabia na misimamo yenu ili iendane na matakwa ya penzi lenu ni jukumu la wote wawili, sio la mmoja. Nakushangaa wewe ambaye kila siku unamsumbua na kumsimanga mwenzako kuwa habadiliki wakati wewe haujawahi kubadilika hata nukta moja. Unalalamika sana nibadilike, sawa!! natamani kuona motisha wa mfano wa kubadilika kwako pia, sio mimi ndio wa kustahili kubadilika wakati wewe ndo mashine ya kubadilisha wengine. Kwenye mahusiano sentensi ya “badilika” haina matunda mazuri na yanayodumu sana kama sentensi ya “tusaidiane kubadilika”. Mabadiliko ni kijitoa “sacrifice” sasa kama na wewe hutaki kushiriki mchakato wa kusaidiana katika kubadilika basi hutaki ku “sacrifice” na kwa kushindwa kufanya hivi ni aidha uchague kuwa ndani yahilo penzi au nje. Adapt or Die – You sacrifice or you suck off-

Via Chris Chris Mauki

WIKIENDI NJEMA WADAU

Next Post Previous Post
Bukobawadau