Bukobawadau

MACHACHE KUHUSU KARAGWE NA WANYAMBO

 Hii ni  barabara  ya kinyinya wilayani Karagwe.
Karagwe imekuwa ikitajwa kwenye vitabu vya kihstoria kama eneo lililokuwa na utawala wa kistaarabu,eneo lilikuwa na ujuzi wa kufua chuma,eneo lililokuwa na njia za utumwa na kituo kikubwa cha biashara kati ya burundi,kongo,rwanda,uganda na pwani ya A/mashariki.kiufupi huu ni mji wa zamani sana.Nimekuwa nikipita mtaani na hata shule nilizosoma na vyuoni nimekuwa nikiulizwa maswali mengi juu ya WANYAMBO wa KARAGWE.Wengi wamekuwa wakiuliza je,Wanyambo ni wahaya?au wanyambo ni kabila linalojitegemea?je mkoa wa kagera wote ni bukoba?au kinyambo ni tofauti na kihaya?.Karagwe si sehemu ndogo ya kabila la wahaya kama wengi mnavyodhani,karagwe kwa asili ni wilaya ya kabila la wanyambo (Ab'hanyambo) na lugha yetu ya kinyambo(orunyambo) kutuita wahaya ni kutunyanganya haki yetu ya msingi ya kuwa na kabila huru na tunaojitegemea. Kuna wahaya wachache waliohamia karagwe hasa huko Nkwenda ktk harakati za kutafuta makazi na udongo wenye rutuba.upo ushahidi wa kutosha wa maandishi na kisanyansi unaoelezea kabila letu la wanyambo na jinsi mwingiliano wa makabila ulivyokuwa.karagwe kuna koo (enganda) kama vile Abeilili,Abaunga,Abagala,Abasindi,Abasita,Abagae,Abasonga,Abayango,Abaimba na wengne wengi sana.kiukweli karagwe ukifika utafurahi sana hasa kimandhari na ustarabu wa Wanyambo.
Wadau wa Karagwe katika hekaheka za hapa na pale

MUHIMU;Wanyambo wanasema kwamba  watu wanapaswa kujua  hata watawala wa zamani kama vile Omukama Ruhinda na Rumanyika tunaowasoma kwenye vitabu ni wanyambo na sio wahaya kama wengi wanavyojua!!!
Bukobawadau  Blogtunaomba mwenye lolote kuhusiana na karagwe atusogezee.

Next Post Previous Post
Bukobawadau