Bukobawadau

MADIWANI MULEBA WAMUWEKA KITIMOTO MAMA ANNA TIBAIJUKA

Na Ashura Jumapili

MADIWANI wa Halmashauri ya Muleba, mkoani Kagera, wamhoji mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka, kuhusu kuziacha fedha za jimbo sh milioni 52 katika akaunti bila kuzitoa wakati kuna mahitaji muhimu yanayohitaji fedha katika jimbo hilo.
Diwani wa Kasharunga, Khalid Hussein (CHADEMA), alihoji kwa nini fedha ziendelee kukaa benki bila kutumika wakati kipindi hiki kata nyingi zinahitaji kujenga vyumba vya madarasa kwa ajili ya wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.
Hussein alimtaka Tibaijuka ambaye pia ni Waziri Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kutoa fedha hizo, ili zisaidie katika kata za jimbo hilo kwa mahitaji muhimu, ili kuboresha mazingira ya utoaji na upatikanaji wa elimu.
Akijibu tuhuma hizo, Tibaijuka alisema fedha hizo ni  kidogo, hivyo haziwezi kutosha katika kata 235 za jimbo hilo huku akidai mfumo wa serikali za mitaa hauna taratibu za kuwezesha  (WDC), hawana hazina wakihitaji fedha hadi waenda kwa mkurugenzi wa halmashauri.
Alisema kutokana na utaratibu huo aliandika barua kwa Waziri Mkuu, ili fedha hizo za jimbo zipitie kwa madiwani kwa ajili ya kuchochea maendeleo.
Alisema diwani ni Mwenyekiti wa Maendeleo na Kata ni ofisi sio mtu huku akisema wenyeviti wa vijiji ni wajumbe na sheria inawatambua wao sio madiwani.
Alisema hoja hiyo alilazimika kuipeleka kwa Waziri Mkuu kwa sababu ujenzi wa chumba kimoja cha darasa ni sh milioni moja, hivyo milioni 52 haziwezi kutosha kwa kata 25.
Baada ya majibu ya Profesa Tibaijuka, Diwani wa Muleba, Hassan Millanga (CUF), alisema utaratibu wa fedha za mfuko wa jimbo madiwani hawakushirikishwa.
Millanga alisema Muleba Kaskazini wanatumia fedha hizo iweje kusini wasitumie wakati zimeletwa kwa ajili ya kuchochea maendelea ya jimbo na kuhoji kata zilizokopa zitapata wapi fedha za kulipa mikopo.
“Kama waziri ana mpango mzuri wa kuboresha matumizi ya  fedha hizo na huo ni mpango wa kitaifa, kwa nini fedha hizo zisiendelee kutumika wakati akiendelea na mkakati wake?” alisema Millanga.
Alieleza hakubaliani na kauli ya Profesa Tibaijuka kuendelea kulimbikiza fedha benki wakati wananchi wana shida
Chanzo;Tanzania Daima.
Next Post Previous Post
Bukobawadau