Bukobawadau

TUMEPOKEA KWA MASIKITIKO KIFO CHA DR SENGODO

Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia JANA alasiri nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanaosadikiwa ni majambazi.
Mwanamageuzi wa kweli,
Mwanaharakati mahiri
Mwanazuoni uliyebobea!

Umekufa kazini,
Ukisimamia mabadiliko yakini.
Umeondoka wakati ambapo mchango wako bado unahitajika sana.

Binafsi siko tayari kukubali kwamba umetutoka.
Najua kifo ni mepenzi ya Mola 
Lakini kwa wewe wamekuwahisha sana. Tanzania bado ilikuhitaji sana.

Kwa umasikitiko makubwa
Umeuawa na watu uliowapenda 
Umeondoshwa na watu uliowapigania!...

Umevipita vita vilivyo vizuri, 
Harakati umezilinda
Mwendo umeumaliza!

R.I.P my Hero!


Next Post Previous Post
Bukobawadau