WILAYANI BIHARAMULO WAHITIMU WA ELIMU WAASWA KULINDA MAADILI
Na Shaaban Ndyamukama November 17, 2013
Wanafunzi wa katoke seminari
Mapadre, katika Misa takatifu kama sehemu ya mahafali
BIHARAMULO: Wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimuwametakiwa kutumia maadili waliyopata katika shule zao kulinda Amani na kuleta maendeleo kwa kutumia taaluma zao ikiwa ni pamoja na kujiendeleza kuongeza ujuzi na maarifa.
Mkuu wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Bw Richard Mbeho ametoa wito huo Nov 16 katika mahafali ya 40 ya wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya seminari ya katoke inayomilikiwa na jimbo katoliki la Rulenge mkoani Kagera.
Bw Mbeho amesema kuwa pamoja na kutumia taaluma mbalimbali hawana budi kuwa makini na utandawazi kwenye mazingira yao kwani unaweza kuchangia kujiingiza katika vitendo viovu na kuhatarisha usalama wa maisha yao.
“Jiepushe na rushwa kwa kutaka mali, madaraka,ngono na hatimaye kujiingiza kwenye vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalamana Amani kupitia njia za utandawazi”.Alisema Mbeho
Amewahimiza na wahitimu kujiendeleza kitaaluma na wazazi kuendelea kutoa malezi kwa watoto wao ili waendelee kutegemewa na taifa kwa kutoa huduma mbalimbali ndani ya jamii zao.
Awali katika ibada ya misa kwa wahitimu hao mkuu wa shule ya seminari ya katoke padre Frolian Tuombe amesema shule hiyo inatoa masomo yote yakiwemo ya ya kiroho kwa kulinda maadili i kwa nadharia na vitendo
Padri Tuombe amewataka wahitimu kufanya kazi kwa uadilifu kwa mujibu wa Imani yao kwa kuzingatia utii wa sheria kanuni za utumishi na kuwajibika bila kwa kulinda haki pasipo kuwa na uonevu wala ubaguzi wa aina yoyote
Katika mahafali hayo zaidi ya Tsh mil 2.59/- zimechangwa na wazazi wa wanafunzi waliohitimu kidatocha nne mwaka huu katika shule hiyo ambapo fedha taslimu ni Tsh 775,200 ili kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili jumuia ya shule.
Mkuu wa wilaya akiwa na Mkuu wa Seminari ndogo ya KatokeWanafunzi wa katoke seminari
Mapadre, katika Misa takatifu kama sehemu ya mahafali